Ijumaa, Desemba 30, 2011

Michezo ina umuhimu gani katika maisha yetu.


Katika pozi Ben Mwanantala mtangazaji wa kipindi cha michezo na burudani kutoka Passion FM Radio nimezungumza naye leo na kumuuliza Michezo ina umuhimu gani katika maisha yetu alisema hivi "unapozungumzia michezo katika maisha ya binadamu basi ni wigo mkubwa zaidi katika kutambua umuhimu wake,kwanza kuwa na afya ambayo itakupelekea usiwe na magonjwa ya mara kwa mara,kuwa mkakamavu sio legelege wakati wote, na kama haitoshi michezo husaidia kupunguza uzito hasa kwa wale mabonge wasio penda kufanya mazoezi,lakini pia mchezo unaweza kuufanya kama mazoezi na ajira kwa wakati mwingine,hivyo ushauri wangu kwa wadau tupende kushiriki katika michezo ya aina mbalimbali

Kijana hapa aliniambia anakaza buti kwa mwaka ujao watu watarajie makubwa katika kipindi cha michezo na burudani kutoka Passion FM

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom