Alhamisi, Januari 26, 2012

Hivi ni kitu gani kinapelekea baadhi ya watu kuchunguza mahusiano ya wawili wapendanao??

Katika safari ya mahusiano ya kimapenzi kuna vitu vingi hujitokeza vizuri na wakati mwingine vibaya na katika hili kuna baadhi ya watu ambao wanapenda sana kuchunguza mahusiano ya watu wengine huku wakitaka kujua ndani ya uhusiano huo kuna nini?? kwa mfano unakuta mtu anachunguza mambo ambayo mwanamke au mwanamume anamfanyia mpenzi wake kama amempa zawadi,,ametoka naye,,anawasiliana naye vipi mwanzoni alikuwa na uhusiano na nani?  anakula nini?? yaani mwingine atataka kujua hadi mambo ya chumbani yanafanyika vipi??

Ukweli ni kwamba huo ni umbea uliokithiri ni vyema kuwa makini nakufanya mambo ya maendeleo kuliko kuchunguza mahusiano yasiyokuhusu mwisho wa siku utaumbuka na mara nyingi watu hawa huwa ni wivu ama chuki inawasumbua hivyo hawapendi kuona wawili wakipendana . NI VYEMA KUTAFAKARI MAISHA YAKO KULIKO KUKAA NA KUWAZA KUMCHUNGUZA FULANI ANAFANYA NINI.......

Maoni 3 :

Simon Kitururu alisema ...

Katika hilo mie nahisi kila mtu ana lake.


Kuna watakao kujua ili kujifunza kitu kwa kuwa wanaona kwa wapendanao kuna zuri.
Kuna wambea na wenye majungu wanataka kujua ili kujisikia vizuri kwanza kuwa hakuna lolote la ajabu liendealo na pia kujikoki ilikuharibu mahusiano ili wapendanao wakiharibikiwa nao wajisikie vizuri kuwote mahusiano mabaya.

Na kuna wadadisi tu kisa wana muda!

Kuwa BIZE utastukia hata muda wako kivyako hautoshi!:-(

Ni Mtazamo wangu!

Bila jina alisema ...

asante sana Simon kuna wengine wanaweza kujifanya wema wanataka kujifunza lakini kumbe wana nia ya kutaka kuharibu kabisa pamoja san

ADELA KAVISHE alisema ...

yaani mimi wananikera sana watu wa tabia hii ya udadisi tena atakuchunguza wakati mwingine anajifanya rafiki yako kumbe mwisho wa siku anakuzungumzia kwa watu vibaya mno haipendezi kiukweli nashukuru sana wadau

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom