Alhamisi, Januari 26, 2012

Inasikitisha sana haya matukio ya ubakaji "mwanamke afa baada ya kubakwa kwa zamu"

Matukio ya ubakaji yamekuwa yakikithiri kila kukicha ijapokuwa serikali inachukua hatua kali dhidi ya jambo hili huko Songea watu watano wanasakwa na polisi kwa tuhuma za kumbaka mwanamke kwa zamu hadi kufa.Kamanda wa polisi Mkoa wa Ruvuma  Michael Kamuhanda  amethibitisha kutokea kwa tukio, hilo ambapo amesema baada ya watuhumiwa hao kumbaka mwanamke huyo kwa zamu hadi kufa walichukua mwili wake  kutoka nyumbani kwake na kwenda kumtupa kwenye shamba la migomba.

Watu waliokuwa wakipita eneo hilo walishtuka kuona mwili huo ukiwa umelazwa katika shamba na kutoa taarifa kwa viongozi wa serikali za mitaa , baadaye askari walienda eneo la tukio wakiwa wameongozana na daktari na kuuchukua mwili huo baada ya  uchunguzi ilifahamika mwanamke huyo alikuwa na michubuko sehemu za siri iliyotokana na kubakwa kwa zamu na watu hao. Polisi wanaendelea kuwasaka watuhumiwa hao na kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo.

Jamani matukio kama hayo yamekuwa yakijitokeza kwa watoto na wakubwa sasa hata kama labda ni kisasi au ni ugomvi haiwezekani  mtu kufanyiwa ukatili wa hivyo sijui adhabu inayotolewa na serikali ni ndogo yaani inasikitisha sana.

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

Ama kweli dunia inakwenda mwisho hakuna wakuaminika kabisa tuwaangalie watoto wetu jamani kwa makini sana na tujaribu kuwachukunguza kila turudipo nyumbani kwa wale wanaofanya kazi na kuacha watoto kwa siku nzima.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom