Nimewaza jambo hili baada ya kukutana na kaka mmoja ambaye alisema " Mpenzi wangu huwa anatabia ya kunikwaza na dharau pale ninapomwambia mambo ya muhimu na tabia yake ya kunisema mbele za watu huwa inanipelekea mimi kumpiga vibao yaani kuna kero ambazo mtu unashindwa kuvumilia na kujikuta unampiga" Jamani kweli inawezekana mtu una hasira kutokana na kero za mpenzi wako lakini sizani kama ni njia sahihi kumpiga kwasababu haisadii lolote bali huongeza matatizo njia nzuri ni mazungumzo na kuwekana sana nini unapenda na nini hupendi au MNASEMAJE WADAU,,WEWE UNALIONAJE HILI KWA MTAZAMO WAKO |
Maoni 4 :
mapenzi hayataki hasira bora muwekane chini tu mzungumze ukimpiga si ndio chanzo cha kumjengea chuki
mimi nampenda sana mpenzi wangu nikimkosea tu mimi ananipiga kwa maneno unaweza ukapewa maneno wwe mwenyewe hadi ukatetemeka mapenzi raha jamani mkielewa tujifunze kumaliza tofauti ili mapenzi tuyaone matamu jamani
yaani mimi simpendi mwanamume anayepiga
yaani mimi mwanamume akinipiga tunaachana
wanawake wengine inabidi kuwapiga jamani kuna wanawake wanadharau sana
Chapisha Maoni