Jumatano, Februari 15, 2012

"sikukuu ya Valentine nilitegemea ningekuwa na mwenza wangu cha ajabu simu yake ilikuwa haipatikani leo ananipigia ananiambia alipata dharura "

Jamani mimi ni mwanamke naombeni ushauri huyu mwanamume nahisi ananidanganya siku ya valentine aliniahidi tungekuwa pamoja, cha ajabu simu yake ilikuwa haipatikani nilihuzunika sana sasa leo ananipigia simu anasema alipata dharura alikuwa nje ya mji, ukweli mimi iliniuma na kuamua kwenda nyumbani kwake kwani funguo ya nyumbani kwake ninayo nilichokikuta ni zawadi zimetoka kwa mwanamke ikiwemo kadi na vitu vingine aliporudi na kunikuta nimeingia naangalia hivyo vitu amekuwa mkali na kusema ni vya rafiki yake. 

Nilimuuliza, kama ni vya rafiki yake vinafanya nini hapo? akanijibu rafiki yake alishinda hapo sikumuamini nikamwambia anipe namba ya huyo rafiki yake nimpigie kumuuliza alikasirika na kusema eti nataka kumuaibisha kwa rafiki zake kuwa mimi simuamini na namuona yeye malaya yaani roho inaniuma sana kwa jinsi ninavyompenda sijui nifanyeje

Maoni 12 :

Unknown alisema ...

DUUU,KWELI HUYU ATAKUWA NO SO IN TO YOU MY DEAR,,MWANAUME KAMA HUYU MUACHILIE MABLI ,KWANI HUJAOLEWA NAE ,KWA HIYO YOU CAN ALWAYS GO AND LOOK FOR A BETER PERSON AMBAE ATAKUJALI HASA SIKU HIZO ZA HUHIM, VALENTINES DAY ,BIRTHDAYS ,XMAS ,AND KWA UJUMLA SIKU KUU ZA MUHIM...POLE DEAR.

Bila jina alisema ...

jamani pole ila mmmh fikiria mara mbili na pia endelea kumchunguza usije umizwa zaidi ya hayo

Bila jina alisema ...

uongo mwengine hata hauelekei.huyo mwanamme amekudanganya.amua mwaya,hajakuoa hali hiyo

lulu ibrahim alisema ...

mhhhhhhhhh shosti mapenzi ni matam sana kama ukiwa na mwanaume mnayependana na kuwa pamoja kwenye kila jambo kama kapata dharula simu alizima ya nini shosti unaibiwa jiepushe mapemaaaaa

emuthree alisema ...

POLE SANA...

Bila jina alisema ...

Jiengue fastar, tapeli huyo kashapata kitu kipya ndiyo maana anaenergy hata ya kukutukana. Work-up and smell the coffee babe

Bila jina alisema ...

Acha kulialia bibie!!! Jambo dogo tu hilo unakimbia nalo blogini kwani alichokuambia hakitoshi? Mbona utahangaika sana na mambo hayo maana usipojua namna ya kujituliza mwenyewe na kuongea na umpendaye usidhani kwamba mahusiano ni mtelemko tu.Mimi sidhani kama ulipaswa uje hapa, maana tutakuchanganya sana.Kwani sisi tulikusaidia kukutongozea huyo mwanaume?mbona mambo mengine yote mnayamaliza na mnakubaliana kisiri huko,iweje hili dogo tu la mara moja ukimbilie blogini?

Kumbuka humu blogini kuna wanawake wenzio wengi hawajapata wapenzi hivyo wanatafuta nani aachike halafu wale bifu lako.Ongea na mpenzi wako yamalize siyo kulialia kama watoto wadogo, wewe hadi umepewa ufunguo wa home kwake bado unahangaika na vitu vidogo hivyo??

Halafu hadithi yako wala haileti maana.Umesema kwamba mlikubaliana kuwa pamoja, lakini hakutokea mahali ulipokuwa,hatimaye ukaamua kumfuata home, hukumkuta na yeye akaja home akakukuta, na huku unasema namba yake ya simu ilikuwa haipatikani, tena unasema leo ndo anakupigia?? na alikukuta nyumbani hii imekaaje,hadhithi zingine za kutunga tu jamani!!!

Bila jina alisema ...

pole dada ila nakushauri sepaa haraka hapo hakuna chako. kwa kawaida no za wapenzi wetu na watu wengine wa karibu yetu huwa tunazo kichwan ama tunaandika sehemu in case ikitokea la kutokea. ss huyo pamoja na hyo dharura ya kwenda nje ya mji alishindwa hata kutumia simu ya kibandani kukutaarifu aarghhhh!

Maggie alisema ...

Bado upo tu hujakimbia.. Mie hata muda wa kumsikiliza nisingekuwa nao kabisa..

Pole sana anza upya wangu..

dellamarie alisema ...

mwenzangu changanya miguu karne hii bora mwanaume ndio akupende sana bt si wewe umpende sana utakufa kimawazo nshajifunza mengi mie pole mwaya....

Bila jina alisema ...

Watu wana wivu jamani "Eti Kimbia, sijiguu, sijui changanya miguu!! Heee jamani yaani kosa hilo ni kubwa kuliko ukarimu aliompa hadi amepewa na ufunguo? Atampata mwanaume gani ambaye hatakuwa na kosa hata kidogo?na yeye ni malaika kiasi gani hata hajawahi kumkosea?

Acheni kumchanganya mwenzenu mpe ushauri wa maana. naungana na msemaji wa pale juu aliyekulaumu kukimbilia humu blogini kuleta ishu ndogo kama hii.

Bila jina alisema ...

asanteni sana kwa ushari mimi naitwa Ashura ndiye niliyeomba ushauri ni kweli nichokisema aunt unayesema ni jambo dogo siku hiyo nilipoenda kwake yeye alikuja na kunikuta nyumbani kwake nikiwa naangalia vitu alivyotumiwa ndipo alianza kuwa mkali na kukanusha na kwa sasa anachoniambia kuwa ananipenda lakini bado anapinga hana mwanamke mwingine zaidi yangu na zile zawadi si zakwake kiukweli moyo wangu haumuamini tena kwasababu namuona ni muongo bora angekubali kosa aniombe msamaha lakini bado ananidanganya asanteni sana kwa ushauri mapenzi yanauma jamani ili si jambo dogo

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom