Mimi ni mwanamke nimepata mchumba tunapendana sana lakini tatizo ana masharti hapendi mimi nivae kimini, au skin tight anataka nivae magauni makubwa na sketi ndefu cha ajabu wakati ananitongoza alikuwa akivisifia sana vimini na nguo ninazovaa lakini kwa sasa anasema hataki kuniona nikivaa nguo hizo inaniuma kwasababu ni nguo ninazozipenda na ninakuwa huru nikivaaa hivyo yaani kila mara tunagombana kwasababu ya nguo naombeni ushauri jamani kwasababu nikimuuliza kwa nini hapendi anasema eti naonekana kama kahaba, ushauri wenu wadau wa blog ya Adela |
Maoni 6 :
Ni wanaume wato wako hivyo na haswa akiwa anawivu kupindukia.Hataki mali zake watu wazione hovyo hovyo.Wanadhani tunataka kuwavutia wengine.yapo mavazi ya heshima na mtu bado unaonekana sex tu.mwenzio pia ninapitia hali kama hiyo na ni mume wangu wa ndoa,inabidi uwe na busara katika hilo kwani utaanzisha mgogoro usio na msingi na bila sababu.
pole sana dada,wanaume huwa ndo walivyo,mara nyingi huisi wanaibiwa mali zao ila jaribu kuongea naye taratibu ipo siku atakuelewa
Mi nakushauri ufuate yale anayotaka yeye, kipindi anakutongoza ulikuwa unamvutia na hivyo vimini lakini kwa sasa upo naye kila akikuhitaki hivyo anakupenda na hataki tena akutamani mtu mwingine, mwanaume yeyote akiona kimini anatamani kwani kinaonesha sehemu za mhimu zaidi ktk mapenzi!!
wewe dada embu jitulize huko wewe umeshapa mtu anaekupenda nawewe unampenda achana na vimini mridhishe mwenzako..kaaa nyie wanawake bwana
Inaezekana kabisa ikawa ni suala la wivu kwamba hofu inakuwa kwamba utawatamisha wanaume wengine kama ambavyo yeye alivyokuona na kisha kuvutiwa nawe.
Sasa cha muhimu umesema kwamba huyu jamaa ni mchumba bila shaka mkiwa na malengo ya kuoana. Sasa ni vizuri kwamba umeshamjua mume mtarajiwa anapenda nini na hapendi nini.Ndoa ni taasisi ambayo inahitaji busara na hekima. Haihitaji ubinafsi hata kidogo.Nitarudi baadaye!!!!
duuu pole sana dada uwo ni wivu tu. we komaa nazo atazoea tu
Chapisha Maoni