Katika mapenzi kuna mambo mengi ambayo ukiyaangalia kwa umakini lazima utagundua kama mwenza wako anakusaliti, yaani ameanzisha mahusiano ya kimapenzi na mtu mwingine inawezekana kugundua haya kwa kuangalia namna anavyoongea na simu je huwa anakuwa katika mazingira gani? mfano: anapigiwa simu mkiwa mmekaa wawili ananyanyuka na kwenda kuongelea sehemu nyingine, lazima utafakari "Hivi huyu mtu kwanini? ameshindwa kupokea simu mbele yangu"
Au mwanzoni alikuwa yupo huru sana na simu yake anaweza kuiacha sebuleni hata popote pale mazingira ya nyumbani, lakini mara ghafla anaanza kuwa makini na simu yake hadi kufikia hatua ya kuingia nayo bafuni huku akijidai anatarajia kupigiwa simu na mtu muhimu,,kuna mambo mengi sana ukiwa makini utagundua katika tendo la ndoa inawezekana akapunguza ubunifu kutokana na kuchoka sana kwa kuwa anao wapenzi wengi,,mazungumzo na mambo mengine mengi KUWA MAKINI MULIKA MWIZI WA MAPENZI,,,,, |
Maoni 5 :
Je, maumbile yake yanaweza kubadilika mara kwa mara kwa mwanamke?
Simu zina mambo yake, hebu jiulize labda kuwe na sehemu unayoweza kuyasikiliza yanayoongewa na kila mtu..mabona ungeshangaa...hata yule!
Yaani, kuna wanawake wengine kila dalili tunaziona lakini tumo tu.. nina rafiki ana boyfriend simu mpaka apige yeye asipompigia hapigi ng'o. Na kuna wakati akimpigia hapokei, lakini yumo tu. Mara kibao nyumbani anakuta mara kibanio, hereni na hata vichupi vya mtu mwingine ila ananyamaza. Mara nyingi kwa boyfriend anaenda ijumaa anarudi chuo j3 ila anaweza akatoka mwanaume peke yake jumamosi na jumapili yeye yuko ndani tu kalala, lakinii yumo tu hata hashtuki kwamba huyu ana mwanamke mwingine, hapo hajaolewa ni hivi, akiolewa? Hata kama mapenzi upofu huyu kazidi. mweee
Uaminifu ni jambo la msingi sana lakini ni vyema sana kuwa makini isije ikawa yule uliyempa uhuru na kumuamini sana kutoka moyoni akakuumiza haya mambo yapo sana jsmani ni vyema kutatua tatizo mapema kabla halijawa tatizo sugu
Wapo wanawake ambao hawaamin ukwel unapo waambia ukwel wanadhan ni uwongo hatakufkia hatua ya kukasrka na kukatsha mawasliano kbsa...hawa nao 2nawaweka fung gan?
Chapisha Maoni