Gosbert Njenga mtangazaji wa Passion FM kipindi cha Afro Passion yeye amesema "Mwanamume atabaki kuwa mwanamume hivyo ni vyema mwanamume afanye kazi na sio kujibweteka hata kama mke wako ana pesa kiasi gani na wewe jishughulishe ili kuweka heshima yako mimi naamini mwanamke akiwa mama wa nyumbani ni kitu cha kawaida kwani analo jukumu la kulea watoto pamoja na mume wake na mwanamume kazi yake inakuwa ni kutafuta lakini itokee baba umekaa ndani halafu mwanamke ndiyo akatafute mimi kwangu sikubaliani kabisa, ijapokuwa inatokea hivyo labda mtu uwe ni mgonjwa kiasi cha kushindwa kujishughulisha........haya jamani JE WEWE UNASEMAJE............
Maoni 1 :
dahhh sasa dada yangu kama ndio umeshapata mpenzi ambaye kazi hana mtaji hakuna na mwanamke mtaji pia wakumuweze hamna je itakuwaje utamuacha kisa yupo nyumbani na ukiangali kwa sasa asilimia kubwa ya wanaume waongo alafu unaona huyo ana nia kabisa na wewe je hapo inakuwaje dada adela
Chapisha Maoni