Jumatatu, Machi 26, 2012

Usifiche hisia zako mwambie ukweli unampenda

Mapenzi hayana siri jamani kama unampenda mueleze ukweli kwani inawezekana hata yeye anahisia za mapenzi juu yako na katika hili unatakiwa ukubali kwamba kuna kukubali ama kukataliwa pale ambapo utaweka wazi hisia zako kwa yule unayempenda inapotokea uliyempenda yeye hakupendi basi ni vyema kukubali hali halisi kwasababu kuna baadhi ya watu akimtongoza mwanamke basi akikataliwa huyo mwanamke atakuwa adui yake ataanza kumchukia na hata kumsema vibaya, kufanya hivyo haisaidii lolote ila ni kujenga chuki na kujiumiza mwenyewe.

Pia kuna ile tabia ya baadhi ya wanawake na wanaume kutaka kujionyesha kuwa hana hisia juu ya mwenza wake ili hali moyoni mwake anampenda ila anajidanganya na kauli hii "jamani mwanamke ukimuonyesha unampenda basi utakoma" hii siyo sahihi onyesha hisia zako za mapenzi ya dhati kwa umpendaye na wewe unayependwa basi siyo ndiyo ujibweteke na kumtegea mwenzio ndiyo akuonyeshe mapenzi.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom