Serikali imeshauriwa kuwawajibisha Walimu wanaokiuka maadili ya kazi zao na kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi kutokana na kwamba hali hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa kiwango cha taaluma. Lakini pia kitendo hicho kinachochea kukosekana kwa maadili na hivyo kusababisha wanafunzi na walimu kutoheshimiana shuleni na kuchangia kiwango cha taaluma kuzidi kuporomoka.
Ufike wakati sasa walimu wawajibishwe inapogundulika anajihusisha kimapenzi na mwanafunzi. Akizungumza na waandishi wa Habari Mwenyekiti wa wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo mkoani Kilimanjaro Bw Patrick Boisafi wakati akijibu maswali ya waandishi wa Habari waliotaka kujua nini kifanyike ili kukomesha tabia za walimu wenye mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni