Alhamisi, Aprili 12, 2012

Picha hii na ujumbe huu mzuri wa kuelimisha nimeukuta katika BLOG ya Marehemu Steven Kanumba ukweli ni ujumbe unaoelimisha sana ukiusoma kwa umakini.

Look at this pic careful,,,moja ya vitu tulivyotofautishwa na wanyama na ndege ni Akili ya kujua mema na mabaya,tizama hao ndege na huyo mbuzi hawana akili kabisa lakini wanapendana ndio maana unaona wako pamoja ILA binadamu aliyepewa akili ana roho mbaya sana,katika mafundisho ya YESU KRISTO alisema neno kuu nawapeni PENDANENI.hata uwe na uwezo wa kuhamisha milima kama huna upendo ni bure,mpende jirani yako kama unavojipenda,upendo haujivuni,hauhesabu mabaya,hautakabari,hauhusudu.....nk,1WAKORINTHO 13.Mungu ana akili sana kutuumba kwa mwili huu wa nyama laiti kama angetuumba kwa vioo au sightmirror ili uweze kuona mwenzako anakuwazia nini?anakufanyia nini?anapanga nini juu yako ungekuta ni heri ukaishi msituni na wanyama wakari kuliko kukaa na binadamu,katika tafiti zangu nimegundua kuna dawa mbalimbali mfano ya kichwa,homa,nk Lakini dawa ya Chuki na roho mbaya hakuna,,kama hiki kingekuwa kipindi kama kile cha zamani za Sodoma na Gomora au cha Nuhu ambacho Mungu alikuwa akiadhibu hapo hapo watu wengi sana wangeumbuka hasa wale wanaojifanya wasafi usoni lakini rohoni ni tofauti,Mungu atusaidie sana hasa sisi vijana tujue kusimama katika ukweli na uwazi,tuubebe upendo wa dhati toka rohoni huku mdomoni tukitamka amani ya kweli impendezayo Mungu ili watoto wetu waje watuenzi kwa mazuri na dunia ijivunie uwepo wetu.

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

Nimependa sana ujumbe wako wa leo. Kumbe na wewe unajua kuhubiri?Vizuri sana Adela huo ni ujumbe mwanana.Ni afadhali mtu anipe ujumbe kama huo kuliko kunipa alamsi halafu nikaangamia nayo.Ubarikiwe sana.Ila na wewe dada uko mzuri na macho yako yanarembua hadi unanifanya nizini na wewe kihisia.Punguza makali Adela,bahati mbaya niko mbali na nakuona kwa picha tu.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom