KITABU MALIPO NI HAPAHAPA
MTUNZI ADELA DALLY KAVISHE
ILIPOISHIA “Tumejadiliana
na kukubaliana na baba yako kwamba kuanzia wiki ijayo
Jamal
utakuwa unalala shuleni ili usome zaidi, kwani tumegundua kwamba huku
nyumbani hupati muda mzuri wa kujisomea.” Alimaliza kuongea mama
Jamal.
“Hapana
mama mimi nitabaki na nani? Sitaki kama ni hivyo bora na mimi
nikalale
shule” Alijibu Aisha huku akimwangalia mama yake kwa hasira.
INAPOENDELEA“Haya mama
na wewe tutakupeleka ukalale shule ukiwa mkubwa kama
kaka
yako.” Alijibu Mzee Said huku akicheka na kumnyanyua Aisha.
“Sawa mama
mimi nitakwenda hakuna tatizo na Aisha si atakuwa anakuja
kunitembelea?”
Alijibu na kuuliza Jamal.
“Ndiyo
atakuwa anakuja, ila nataka ukasome kwa bidii ukifaulu vizuri
nitakupa
zawadi nzuri sana, sawa mwanangu.” Alisisitiza mama Jamal.
“Sawa mama
bila shaka nitasoma sana kwanza nataka kuwa Waziri wa
fedha
nikiwa mkubwa.” Aliongeza Jamal.
Baada ya
wiki moja Jamal alihamia shuleni na kumwacha mdogo wake
akiwa na
wazazi wake pamoja na msichana wa kazi. Wazazi wake walikuwa
wakienda
kumtembelea mara mojamoja. Jamal akiwa anaendelea na shule
aliwazoea
wanafunzi na mazingira ya kuishi bweni.
Jamal
alipofika Kidato cha Tatu alikuwa kijana mkubwa mwenye busara
na mwenye
kupenda sana kusoma. Mama yake aliongeza bidii katika
shughuli
zake za kutafuta kipato ili kuhakikisha Jamal anapata mahitaji
yote ya
shule na mengineyo. Mara kwa mara alimtembelea Jamal shuleni
na kumuasa
asome kwa bidii ili kujiandalia maisha yake na ya mdogo wake.
Jamal
alikuwa mtiifu katika kila aliloshauriwa na mama yake.
***************Baada ya miezi sita**********************
Siku moja
mama Jamal aliugua ghafla na kupelekwa hospitali kwa ajili ya
matibabu.
Kutokana na hali yake kuwa mbaya sana mama Jamal ilibidi
alazwe. Mzee
Said alihangaika sana kuhakikisha mama Jamal anapata tiba
bora naya
haraka ili kunusuru uhai wake. Mzee Said aliamua kumfuata
dokta
ofisini ili kutaka kujua kinachomsumbua mke wake.
“Habari
yako Mzee. Karibu sana,karibu uketi”Alisema Daktari baada tu
ya Mzee
Saidi kuingia ofisi.
“Asante
Daktari vipi hali ya mke wangu anaendeleaje.” Alijibu na kuuliza
Mzee Said.
“Hali ya
mkeo inaendelea vizuri ila kuna tatizo ambalo tumeligundua
baada ya
kumpima.” Alijibu Daktari.
“Tatizo
gani hilo Daktari?” Aliuliza Mzee Said.
“Mke wako
ana kansa ya kizazi ambayo inamsumbua kwa muda mrefu
lakini
hakuwahi kwenda hospitali na hili ni tatizo kubwa. Ningependa
kuwa
muwazi kwako, ni kwamba maisha yake yapo hatarini kwani ugonjwa
alionao
umefikia katika hatua mbaya sana.” Alisema Daktari huku Mzee
Said akiwa
anamsikiliza kwa makini.
“Mungu
wangu! Unamaanisha nini maisha ya mke wangu yapo hatarini?
Inamaana
hatopona kabisa?” Aliuliza Mzee Said kwa sauti ya
kuchanganyikiwa.
Daktari
naomba unisaidie mke wangu apone kwa gharama yoyote ile
fanya
uwezalo.” Alisihi Mzee Said.
“Kwa kweli
kwa hatua aliyofikia itamchukua muda mfupi kuishi ila
nitampa
dawa za kutuliza maumivu ili angalau kumwongezea siku za
kuishi.”
Alisema Daktari.
Mzee Said
alikaa kimya kwa muda kidogo huku akiwa hajui atafanya nini,
kisha
alijikaza na kuomba akamwone mke wake. Daktari alimpeleka kwa
mkewe na
kumruhusu kuzungumza naye. Mama Jamal alipomwona tu
mume wake
alianza kububujikwa na machozi huku akimwangalia
mumewe kwa
uso wa kuonewa huruma.
“Mume
wangu naomba unisamehe kwani huu ugonjwa nilikuwa najua
kuwa
ninao, lakini sikukufahamisha nikawa nameza tu dawa. Nisamehe
baba
Jamal.” Alitamka mama Jamal huku akilia kwa kutoa kwikwi.
“Usilie
mke wangu Mungu atakusaidia utapona.” Alitamka Mzee Said
huku
akisogea na kumshika mkono.
Kesho yake
mama Jamal alipewa dawa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Akiwa
nyumbani hali yake ilizidi kuwa mbaya na alitaka mtoto wake Jamal
akaitwe
shuleni ili aje azungumze naye. Mzee Said aliondoka kuelekea
shuleni
anakosoma Jamal.
“Itakuaje
kwa Jamal akigundua kuwa mama yake anaumwa kansa na
hawezi
kupona?” Aliwaza Mzee Said akiwa njiani kuelekea shuleni.
Alipofika
katika ofisi za utawala aliwaeleza walimu hali halisi kuhusu
kuugua kwa
mama yake. Walimu walimwita Jamal.
Baada ya
Jamal kumwona baba yake alishtuka kwani haikuwa kawaida yake
kwenda
kumtembelea shuleni. Je nini kinaendelea usikose sura ya .....3.....
Maoni 1 :
jmn so sad kwa kweli.jamal hakijua mama yake anauwa sijui itakuwaje.
Chapisha Maoni