Alhamisi, Mei 10, 2012

Atuhumiwa kumuua shemeji yake kwa sumu

Chanzo cha Ugomvi uliotokea baina yao ulisababishwa na marehemu kudaiwa kwa muda mrefu deni la sh 320,000 hatua iliyofuatiwa na mtuhumiwa kumchukua mke wa marehemu ambaye ni mdogo wake na kumrudisha nyumbani kwao mpaka deni litakapolipwa. 

Akizungumzia sakata hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Thobias Andengenye amesema   marehemu aliweza kulipa deni hilo na alitarajia kurudishiwa mke wake, lakini wazazi wa mke walimkatalia binti yao kwa kutoridhishwa na tabia ya mume wake jambo lililomfanya ajenge chuki na marehemu kuwa ndiye aliyesababisha mke wake kuondoka na kutorejea. nyumbani kwake. 

Mara baada ya marehemu kunywa pombe hiyo hali yake ilibadilika ghafla na kuomba maji ya kunywa ambapo watu aliokuwa nao walishauri apewe maziwa lakini alifariki kabla ya kunywa maziwa hayo.Kamanda amesema mara baada ya tukio hilo mtuhumiwa alijaribu kukimbia lakini alikamatwa na askari mgambo ambao walimpeleka Polisi na kwa sasa anasubiri kufikishwa mahakamani.

Aliongeza kusema kuwa uchunguzi uliofanywa na daktari wa Hospitali teule ya Wilaya ya Ngorongoro umeonyesha kuwa marehemu alikunywa sumu lakini hata hivyo sampuli za vipimo zaidi zimepelekwa kwa Mkemia mkuu wa serikali kwa uchunguzi zaidi.

NI VYEMA KUTAFAKARI KABLA YA KUTENDA

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom