|
Imesemekana kuwa Watu wanaokula Chocolate mara kwa mara huwa wembamba. Hii ni kwa
mujibu wa utafiti mpya. Karibu watu 1000 nchini Marekani walifanyiwa
utafiti ambao wamekuwa makini katika vyakula vyao. Waliokuwa wakila Chocolate mara kwa mara
walipatikana wakiwa wembamba kuliko wenzao ambao hula Chocolate baada ya
muda.
|
|
Wanasayansi wanasema, japo Chocolate ina sukari nyingi, ina viungo
ambavyo husaidia kupunguza uzito wa mwili, lakini siyo kuchoma mafuta. |
|
Hii siyo mara ya kwanza wanasayansi wameelezea
umuhimu wa Chocolate. Utafiti wa awali umeonyesha Chocolate inasaidia
ugonjwa wa moyo.Baadhi ya chocolate zinasaidia kupunguza msukumo wa damu, kiwango
cha sukari mwilini pamoja na mafuta. |
ONYO:: Kuwa makini na Chocolate
unayoila kwani baadhi zina sukari na mafuta mengi.Ikiwa unataka kuwa na
afya bora, jaribu kula mboga na matunda mengi ujumbe huu kwa msaada wa BBC Swahili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni