Mkazi wa kijiji cha Olkeijulongishu Wilayani Longido Mkoani Arusha, aliyefahamika kwa jina la Bi. Neisisiri Mokoroo mwenye umri wa miaka 25 amefariki baada ya kupigwa na mumewe kwa tuhuma za kuwa na ujauzito ambao anadai si wake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Bw. Liberatus Sabas amesema tukio hilo limetokea katika wilaya ya Longido amesema Marehemu alikutwa na mauti baada ya mumewe aitwaye Kapaito Naanjarati. kudai kumshambulia mke wake kwa kumpiga na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake hali iliyomsababishia kifo chake.
Kwa mujibu wa taarifa za awali zilieleza kuwa tukio hilio lilitokea bada ya wanandoa hao kwenda shambani kukata nyasi na walipofika huko ndipo mtuhumiwa alipomuua mkewe.
Baada ya tukio hilo mtuhumiwa alikimbia kuelekea kusikojulikana na kuwa polisi wanaendelea na msako. Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Longido na uchunguzi unaendelea. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni