Jumanne, Juni 12, 2012

JE INGELIKUWA NI WEWE UNGEFANYAJE

Sara alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na kijana Juliasi ambaye alimnyanyasa sana katika mapenzi alikuwa akimsaliti na hata kumpiga mara kwa mara kutokana na misukosuko katika uhusiano wao Sara alichoka na hata ndugu na jamaa walimshauri aachane na huyo mchumba wake, wakati Sara akiwa na mchumba wake huyo kuna kaka mwingine anaitwa John alikuwa akimpenda sana Sara na siku zote alikuwa anatamani siku moja Sara aje kuwa mke wake.

  Baada ya Sara kuachana na Juliasi haikupita muda ndani ya mwezi mmoja alianza uhusiano na John na mapenzi yakawa motomoto sasa wakiwa katika pilikapilika za kutaka kufunga ndoa Sarah anagundua kwamba ni mjamzito na mimba hiyo ni ya Julias na katika kucheki ina miezi miwili na hapo alipo yupo kwenye pilikapilika za kufunga ndoa na John JE ATAFANYA NINI?? Kama ingelikuwa ni wewe unafanyaje utamwambia ukweli John au utanyamaza kimya....

Maoni 6 :

DAVID JERMOS alisema ...

yani hapo hakimwambia ukweli huenda na huyo john akamwacha pata potea,tumisha fanya dhambi sana tutamuomba mungu msamaha tu,mi ningekuwa ni sara ningeenda kuitoa hiyo mimba!!

Bila jina alisema ...

Duuuh bora kusema ukweli tu hapo

Bila jina alisema ...

mhmmm mie NINGEMWOMBA Mungu anisamehe then NINGEENDA KUITOA KIMYA KIMYA.

Bila jina alisema ...

kama alimwadithia ya nyuma yaani uchumba wake na julias sidhani kama itakuwa ngumu kwa john kuelewa ila kama hajasema kazi ipo hapo.

Bila jina alisema ...

Kama Sara alikuwa muwazi kwa John kuhusu uhusiaono aliokuwa nao na Juliasi, na kwamba baada ya kuachana na Juliasi hakujua kama ana ujauzito ndo amegundua sasa wakati yupo na John. Basi ni vyema amwambie John ukweli sasa.

Bila jina alisema ...

Kama Sara alikuwa muwazi kwa John kuhusu uhusiaono aliokuwa nao na Juliasi, na kwamba baada ya kuachana na Juliasi hakujua kama ana ujauzito ndo amegundua sasa wakati yupo na John. Basi ni vyema amwambie John ukweli sasa. Na Sara awebtayari kukubaliana na matokeo ya maamuzi ya John.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom