Jumatatu, Juni 11, 2012

Sababu za kuandamwa na chunusi

Mambo yanayosababisha kuwa na chunusi ni pamoja na ulaji wa vyakula vyenye mafuta humweka mlaji hususani mwenye ngozi ya mafuta kupata chunusi, lakini pia kutokula chakula bora kunaweza kukuletea tatizo hilo, jambo lingine ni matumizi ya nguo chafu,mfano kulala kwenye foronya chafu zenye vumbi na mafuta hukuweka kwenye hatari ya kupata chunusi ni vyema kulitambua hili na kuwa makini na usafi unashauriwa kuvaa kofia ya kulalia wakati wa kulala ili kuepuka kuchafua foronya zako pia usijifute na taulo chafu.

Wanawake wengi wanapenda kujishika usoni mara kwa mara bila kuwa na uhakika wa usafi wa mikono yao jambo hili limekuwa likisababisha maambukizo ya bakteria katika ngozi wanaoleta maradhi kama vile ya chunusi na mengineyo, lakini pia kuwa makini unapoosha nywele zako kwani wakati wa kuosha nywele wakati mwingine husababisha mabaki ya mafuta  kuingia usoni na hivyo kuiweka ngozi yako ya uso katika hatari ya kupata chunusi

Pia kumbuka kusafisha uso wako mara kwa mara na kutumia vipodozi sahihi ambavyo umeshauriwa na wataalamu kulingana na aina ya ngozi yako. mwisho wakati wa kulala hakikisha unaondoa vipodozi vyote usilale ukiwa umepaka vipodozi kwani kwa kufanya hivyo utakuwa unakaribisha chunusi

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom