Mkoa wa Dar es salaam umetajwa kuwa unaongoza kwa upande wa Tanzania bara kwa kuwa na vitendo vingi vya wanawake kuwapiga waume zao.Hayo yamebainishwa na utafiti uliofanywa na kituo cha haki za binadamu na utawala bora (LHRC) dhidi ya ukiukwaji wa haki za kijinsia.
Wakili na Afisa ufuatiliaji wa ukiukwaji wa haki za binadamu wa kituo hicho Ntagazwa amesema hayo kwenye mafunzo ya siku tatu ya waangalizi wa haki za binadamu wa mikoa ya Nyanda za juu Kusini ambao walikutana jijini Mbeya.
Amesema vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vipo hata kwenye ngazi ya familia.Amesema utafiti uliofanywa umebaini kuwa mkoa wa Dar es salaam una asilimia 5.3 ya matukio ya wanawake kuwapiga waume zao na kuwa ndiyo mkoa wenye asilimia kubwa zaidi kuliko mikoa mingine yote ya Tanzania Bara kwa matukio hayo.
Hata hivyo amesema kisiwa cha Unguja ndicho kinachoongoza nchini kwa matukio ya wanawake kuwapiga waume zao ambapo utafiti huo uligundua kuwepo kwa asilimia 7.3 |
|
Maoni 3 :
Hii kali jamaa huyo akitoka njeanatamba, mimi mke hanibabaishi...lakini duuh, ...kasheshe. Tupe vitu mpendwa
Na bado tutawakung'uta sana kama mnajifanya wanaume wakati mna behave kama kids.
Hiyo kali inabidi wabadilike vinginevyo kichapo lazima kitembee
Chapisha Maoni