"Baba yangu anataka kumuoa na mama yangu mdogo"
Mimi ni msichana ninaishi na wazazi wangu wote wawili familia yetu hapo mwanzo ilikuwa ni familia iliyojaa upendo na amani tatizo linakuja hivi karibuni baada ya mama yangu mdogo ambaye amezaliwa tumbo moja na mama yangu kuja kuishi hapa nyumbani na kuanzisha mahusiano na baba, mwanzoni mama alikuwa hafahamu kinachoendelea lakini baadaye alipofanya uchunguzi alimfumania na hivyo kuamua kumfukuza pale nyumbani wakati akimfukuza mama Mdogo tayari alikuwa ni mjamzito,
kutokana nna hali hiyo kulikuwa na ugomvi baina ya baba na mama mimi nawapenda sana wazazi wangu zaidi namuonea sana huruma mama yangu naumia sana na namchukia sana mama yangu mdogo na sasa baba anamwambia mama anataka kumuoa mama mdogo kama mke wa pili namuone huruma mama anataka kuondoka arudi kijijini Moshi sijui nifanyeje ili mama asiondoke kwani mimi bado nipo shule kidato cha sita na ninao wadogo zangu wanne bado wanaitaji malezi ya baba na mama naombeni ushauri
Maoni 4 :
Pole sana binti.Yaani nimetokwa na machozi hasa ulipogusia ninyi watoto na idadi yenu halafu mama awe mbali nanyi.Kweli hilo ni gubu jamani.Mama mdogo kuingilia ndoa ya dada yake?Mwambieni baba yenu kama anamuoa mama yenu mdogo asimlete hapo nyumbani ampangishie kwingineko ili mama yenu abaki hapo akiwalea wanawe.Kaa na wadogo zako zungumza pamoja mumwite baba yenu mumueleze athari zinazowakabili kwa hilo analotaka kulifanya na hilo alilolifanya.Na mwambie kama unamuoa mama yetu mdogo amtafutie mahali pengine asikaribiane na mama.msihi mama asiondoke hapo home hadi kieleweke.Pole sana binti.
Pole sana binti.Yaani nimetokwa na machozi hasa ulipogusia ninyi watoto na idadi yenu halafu mama awe mbali nanyi.Kweli hilo ni gubu jamani.Mama mdogo kuingilia ndoa ya dada yake?Mwambieni baba yenu kama anamuoa mama yenu mdogo asimlete hapo nyumbani ampangishie kwingineko ili mama yenu abaki hapo akiwalea wanawe.Kaa na wadogo zako zungumza pamoja mumwite baba yenu mumueleze athari zinazowakabili kwa hilo analotaka kulifanya na hilo alilolifanya.Na mwambie kama unamuoa mama yetu mdogo amtafutie mahali pengine asikaribiane na mama.msihi mama asiondoke hapo home hadi kieleweke.Pole sana binti.
Kesi nzito hiyo, ila kwa jinsi nionavyo mie njia rahisi kwako ni kuwashirikisha ndugu wa karibu wa familia zote upande wa mama na upande wa baba kwani sio tukio la kawaida sana naamini hata wao wakisikia lazima watakuja juu na wataingilia kati.
Kwa jinsi nijuavyo mie kwenye kila familia huwa panakuwa na watu wazima ambao wao ndio wasimamizi wa familia ama ndio wakubwa na wenye sauti kwenye familia zetu nyingi naamini hilo linafanana kwa hiyo peleka suala hilo kwao kwani ni kweli wazazi wakitengana wanao umia ni watoto ambao hawana hatia hata kidogo.
Kila la kheri.
Pole sana, hili ndilo tatizo la ndoa, wanandoa wengi wanakuwa na udhaifu wa ndoa zao.
Nahili huwa mara nyingi napenda kusema kuwa hii ni ile hali ya kuingia kwenye nyanja fulani bila kuijua au kuisomea.
Swali je wewe unaweza kuwa dereva, au dakitari au muhasibu bila kuusomea uhasibu? jibu ni hapana, ili uifanye hiyo kazi vyema na kuifahamu ni vyema ukaisomea.
Sasa swali je wanandoa ngapi ambao kabla ya kuoa wanasomea au kujifunza maswala mazimaya ndoa?
Kiujumla wengi wanakurupuka tu, ilimradi kakua, anauwezo,ana....nini sijui,basi kidume,nataka kuoa, hataki hata kutafiti,ndoa ni nini, ni ninimasharti ya ndoa...
Ndio nakubali siku zile zakuozeshwa kuna maoni, kuna kuelezwa hiki na kile, kuhus ndoa, ni nini, lakini hakitoshi.ilitakiwa kwanza mtu mwenyewe aijue vyema ndoa ni nini.
Ni vyema kabla ya kuingia kwenye hii nyanja yakuitwa mwanandoa, ukajifunza, na kuijua vyema ndoa ni nini,na nifanye nininikiwa ndani ya ndoa, na sitakiwi nifanye nini....
Sasa hapo sijui, kuwa kweli,je imani zinaruhusu mtu kuoa mke na mdogo wake,
pili hata kabla ya kutaka kumuoa..huyo mdogo mtu, huyo jamaa alishavunja masharti ya ndoa,....
Hii nikuonyesha KUWA HUYO JAMAA haikujua ndoa yake,na msaharti yake.
Tatu, kwanini mpaka huyo baba akavutika kwa mdogo mtu, tuangalia hili kwa undanizaidi,kwani wakati unamnyoshea mwenzako kidole, ni bora ukajiangalia wewe mwenyewe kwanza kwani kuna vidole vitatu vinakuonyeshea wewe.
Je kwanini huyo mwanababa akavutika kwa mdogomtu, wengi tutasema ni kwa kujiamini kuwa ni tamaa tu!
Ni kweli hairuhusiwi kuwa na tamaa, hili nalikubali, ila kuna wengine hiyo kinga ya kuishinda tamaa hakuna,....sasa wafanyeje,
Hili ni swala muhimu kwa mke alitakiwa alijue, na dawa ya hilo ni kumshibisha mume wako. Jamani wanandoa angalieni hili swala kwa makini,...kwani tatizo likitokea, nani ataumie, na je kwanini hatukuchukua ahadhari mapema!
Kwasababu ni nini anakitaka huyu mume kwahuyo mdogo mtu, ina maana dada mtu hana hicho kitu? jibu ni kuwa anacho, sasa tatizo ni nini...tuliangalie hilo swala kwa makini, tukijua kuwa kuna udhaifu wa kibinadamu.
KWA USHAURI WANGU: Hasa kwa wewe mleta hoja.
Hilo linahitaji nguvu ya ziada, nikiwa na maana wakubwa wanatakiwa waliingilie kati.
Linahitaji wazee walijadili, wamshauri jamaa, na ikibidi watu wa dini wawepo kulijadili,....
Wewe kama mtoto, kaa pembeni, soma, ili uje usaidie,....kwa hali kama hiyo elimu yako, ndiyo itaweza kusaidia baadaye.
Wakati huu jifanye huoni...jibidishe kwenye elimu yako,maana elimu ndiyo itakayokusaidia na kuwasaidia wadogo zako na mama yako kama lolote litatokea!
Ni hayo tu,...ukitaka kujua hili tatizo landoa, fika kijiweni kwangu na soma kisa kilichopo cha `Hujafa hujaumbika (http://miram3.blogspot.com/) utajifunza mengi.
Samahani kwa kuanza kutunga kisa hapa kwako mpendwa Adela!
Chapisha Maoni