Mimi ni mwanamume ninaishi na mke wangu ambaye kwa sasa tuna takribani miezi nane tokea tulipofunga ndoa nampenda sana mke wangu lakini tatizo ni tabia ya mke wangu kila tunapozungumza lazima atamtaja alyekuwa mchumba wake wa zamani tena mambo mengi anayozungumza ni ya kumsifia nilishawahi kumuambia kuwa tabia yake hiyo siipendi lakini anabaki kucheka na kusema kuwa nina wivu.
Tuliendelea kuishi hivyohivyo nikaanza kufuatilia simu yake ndipo nilipokutana na ujumbe wa kimapenzi kutoka kwa huyo mchumba wake wa zamani naumia sana moyoni mwangu na pia napata hasira sana kwani mpaka sasa sijamuuliza chochote nahisi kutokana na hasira nilizonazo naweza kumuumiza sijui nifanyeje katika hili NAOMBENI USHAURI
Maoni 6 :
PENGINE HUMFIKISHI PANAPOSTAHILI NDO MAANA,INABIDI KABLA YA KUFANYA CHOCHOTE MUULIZE VIZURI ANARIDHIKA MNAPOKUWA SITA KWA SITA?INAWEZEKANA HUYO WA ZAMANI ANA KITU AMBACHO HAKISAHAULIKI
HAKUN LOLOTE SISI WANAWAKE WA SASA TUNAPENDA KUENDEKEZA UMALAYA.. KAMA HUYO ANAMFIKISHA KWA NINI ASIOLEWE NAE?NI BASI TU TABIA MBAY
Tabia chafu; period. Mwambie black and white kuwa hupendi tabia yake; na ajiweke kwenye position yako. Punguza upole. Mimi ni mwanamke nilo kwenye ndoa miaka nane sasa. Sijawahi sikia mwanamke mwenye jeuri ya kusifia ma ex wake kwa mumewe. Utakuwa na kasoro ya upole ulopitiliza maana mkeo ameanzia wapi kubwabwaja kuhusu wanaume wake wa zamani.
Kuna wanawake malaya na wanaotutia aibu sisi wake za watu ambao ni decent maana siku hizi utasiki wanawake nao ni cheaters; isije kuwa na wakwako ni mmoja wa hao wachache. Kambare mkunje angali mbichi; anaku test huyo. Shaulilo.
kaka mie nakushauri anza kusikiliza times fime kipindi cha pilotoc kinachoonza saa nne uck mpka sita,yn utakuja kusema hapa mna naic itakusaidia sana na pia omba kukutana na yule kaka Misana thn umuelezee tatzo lako hatakusaidia au hta ukisikiliza akitoa no zake za simu ukimtumia ujumbe hatakushauri vzr na anahokoa ndoa za watu wengi sana na j2 ya kesho kutwa wana semina ya LOVE CLINIC itakayofanyika lamada hotel so jitaidi kesho usikilize na ukiweza fanya juu chini uwende kwenye semina hayo yani am sure mafunzo utakayoyapat huko au kwa uyo kaka uyo mkeo hatamsahau uyo boi wake wa zamn na utalud kusema huku kma nau mambo safi na mkeo.
Nadhani humpi mapenzi matamu.kama ndio hivyo alikuwa na huyo mwandani bila shaka alikuwa mtundu,kiasi kwamba huyo mama haji kumsahau anapokosa kwako.Lakini hata hivyo huyo mkeo ana tatizo la akili,maana haiji akilini kwa mwanamke ujimwage hivyo kwa mumeo kumsifia mchumba wako wa zamani ambaye hana nafasi kwa sasa.Hilo ni chukizo sana.Ndugu acha upole usio na tija.Mwambie na muonyeshe hata hizo msg za kimapenzi alizotumiana na huyo wake wa zamani.Usipofanya hivyo atakuongezea vituko na utajinyonga.Kuna mtu amekushauri uende kwenye semina, mimi nadhani ukienda wewe peke yako ni sifuri.Lazima uende na yeye mpate wote yatakayowafaa.
Jaribu kuwa mvumilivu kumpiga mkeo ni kosa la jinai unaweza kumpiga akaaumia au kupoteza maisha halafu hasara juu yako angalia ni wapi unakosea ili urekebishe na pia muombe mungu kwa sbb hakuna linalioshindikana kwa mungu ukiwa na iman na uvumilivu
Chapisha Maoni