Jumatano, Agosti 01, 2012

MGOMO WA WALIMU UPATIWE UFUMBUZI



Juzi chama cha Walimu nchini ( CWT) kilitangaza kuanza rasmi mgomo wa walimu nchi nzima.,mgomo huo umekuja ikiwa ni baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya walimu na Serikali ambapo walimu wanashinikiza mambo mbalimbali likiwemo la nyongeza za mishahara na kujengewa mazingira rafiki ya kufanyia kazi.

     Kutokana na mgomo huo imeshuhudiwa wanafunzi katika shule nyingi  nchini wakikosa masomo,baada ya walimu kuweka vitendea kazi chini huku wakishikilia msimamo wao wa kutoingia madarasani hadi hapo matakwa yao yatakapokuwa yametekelezwa.

    Hali hiyo imewafanya pia wanafunzi kujitosa katika sakata hilo kwa kuamua kuandamana hadi mwenye ofisi za watendaji wa serikali ili kuishinikiza serikali imalize mgomo huo na wao waweze kupata haki ya msingi ya masomo.

   Tunaungana na wanafunzi hao kuiomba serikali kukaa na walimu mezani ili kutafuta suluhu ya mgomo huo kwa haraka kwani unaweza kusababisha madhara makubwa katika sekta ya elimu.

    Tunasema hivyo kutokana na kwamba ugomvi huo wanaoathirika ni wanafunzi ambao wanakosa masomo kwani kuna msemo usemao mafahari wawili wagombanapo ziumiazo ni nyasi.,katika ugomvi huo wa mafahari wawili serikali na walimu wanaumia ni watoto wetu.

    Tuna imani Serikali kwa kulitambua hilo itachukua hatua za haraka ,ili kuhakikisha inapata ufumbuzi wa suala hilo kabla watoto wetu hawajaathirika zaidi kutokana na mgomo huo.. 

Maoni 2 :

emuthree alisema ...

Tukumbuke kuwa wakigombana mafahali ziumiazo ni nyasi, na tumeona mara nyingi, migomo inawaathiri sana watu wa chini, kwani ukiingalia hapa wenye nazo watoto wao wapoo shule za kulipiwa, ....!

La Princessa alisema ...

this is really sad

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom