Jumatatu, Septemba 24, 2012

NI VYEMA KUJIPENDA WEWE KABLA HAUJAPENDWA

Katika maisha ili uweze kuishi kwa furaha ni vyema kujitambua  na kujipenda. Binafsi maisha yangu nimejipa kipao mbel sana yaani najipenda mimi kabla sijapendwa ni vyema kufanya hivi kwasababu  UTAISHI KWA KUJIAMINI  kwani kuna baadhi ya watu wanadiriki kujichukia na kujiona hawafai katika hii dunia mwingine anadiriki kumkashifu  Mungu kwa maisha aliyonayo. JAMBO LA MSINGI NI KUJITAMBUA KUJIPENDA NA KUSONGA MBELE  BILA KUKATA TAMAA
n

Maoni 3 :

emuthree alisema ...

Bibi yangu siku moja alikuwa akitupa hadithi zake, na siku hiyo akawa kavalia vizuri sana, akatuuliza;

'Eti jamani ni nani mnzuri sana hapa dunia?'
Tulishidwa kujibu, maana sisi wakati huo ni watoto wadogo, na hawo wanaoitwa warembo, au miss world hatuwajui,tukasema hatujui.
'Jamani hata mimi sio mzur'?' akatuuliza.
Basi kwa kujipendekeza tukasema ;
'Ni wewe bibi'
'Mumekosa'akasema kwa sauti ya juu, na akadai tumpe mji, na hata mji tuliompa akasema hautaki, mwishowe mmoja akagundua na kumpa mji wa pale kijijini.
'Safi kabisa, huondio mji wangu'
Jibu lake, mrembo kuliko wote duniani ni wewe mwenyewe, kama ni msichana kama ni mvulana halikadhalika maana hata wavulana wanashindana urembo wao sijui wanauita nini.
LEO nimejua kwanini bibi alisema hivyo,ndio hata wewe mpendwa Adela umelithibitisha hilo
Mtu akikuuliza mrembo kuliko wote sema ni `wewe mwenyewe' ndio maana unajiangalia kwenye kiyoo kila siku,maana unajipenda, jamani kuna ambaye hajipendi?

Bila jina alisema ...

Kweli unayosema bila kujitambua na kujituma huwezi kufanikiwa. Leo ndio kwanza naiona blog yako kumbe ina mambo mazuri sana kama we mwenyewe! Usikate tamaa endelea kujituma bila kuchoka utapata mafanikio zaidi ya uliyonayo.

ADELA KAVISHE alisema ...

asanteni wadau wangu tuko pamoja

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom