"Sikuwahi kufikiri kama mwanamume ninayempenda anaweza kuniumiza kwa kiasi hiki" hayo yalikuwa maneno ya Sara aliyekuwa anawaza baada ya kumfumania mpenzi wake aliyekuwa anampenda kwa moyo wake wote na tegemeo lake siku moja wangefunga ndoa. lakini kutokana na tabia za mpenzi wake malengo hayakutimia na Sara kuamua kuolewa na mwanamume ambaye wazazi wake walimchagulia katika maisha yake mapya mwanamume aliyemuoa alikuwa akimpenda na kumjali Sara kwa kila kitu
lakini cha ajabu siku moja Sara alikuja akakutana na yule mpenzi wake wa zamani kumbe bado alikuwa na mapenzi naye wakaaanzisha mahusiano ya siri huku Sara akiwa tayari ni mke wa mtu ukweli ni kwamba za Mwizi ni arobaini sikumoja mume wa Sara alikuja akamfumania Sara na hapohapo akamua kuachana naye huku Sara akiwa ni mjamzito mume wake aliikataa mimba na hata yule jamaa yake wa pembeni naye alikataa mimba Sara alirudi kwa wazazi huku akiwa hajui nini hatima ya maisha yake. JE UNAFIKIRI NI KWANINI SARA ALIAMUA KUTOKA NJE YA NDOA YAKE???????????/
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni