Mimi ni mwanamume nina mke na watoto watatu, naipenda sana familia yangu lakini tatizo lipo kwa mke wangu anapenda sana kuhudhuria katika sherehe mbalimbali hakuna sherehe itakayompita kiasi kwamba naona hata kazi anashindwa kufanya inawezekana kila siku yupo kwenye vikao vya kitchen party mara harusi yaani tokea nimemuoa hii tabia imeanza ina mwaka mmoja nimeshawahi kumkalisha chini na kumshauri lakini naona tabia hiyo inaendelea inanikera sana kwani naona hana muda hata wa kukaa na watoto zaidi ya kuwaza sherehe yaani natoa michango ya hizo sherehe majina mengine siyajui ila yeye ananiletea kadi yakutaka mchango nimechoshwa na hii tabia NAOMBENI USHAURI JAMANI. Kwani amekua akitoka kwenda kwenye sherehe kila weekend na kurudi usiku wa manane.
Maoni 4 :
Mimi huwa napenda kusema hivyo kuwa mnapooana mnakuwa kitu kimoja, na kama mmoja anakuwa kivyake, ni kuivunja ndoa kwa mikono yake.
Ni vyema kuwa pamoja, kukubaliana ,na hili linatakiwa kuongea ,kujadiliana, na kuwa na mipango ya pamoja.
Familia kama office inahitaji bajeti, yaani kila wiki mnakaa mnapanga matumiz ya wiki, na mnakubaliana, kutegemeana na kipato chenu.
Sasa hiyo mipango isiyokuwepo kwenye makubaliano haihitajiki ,labda iwe ya dharura.
Mpange mkeo muwe na utaratibu kama huo,ili muweze kuratbi shughuli zenu za mara kwa mara, na kupunguza safari, au michango kama hiyo ambayo haipo kwenye makubaliani,labda kama mwenzetu una kisima cha pesa....NI WAZO LANGU KWA LEO
Kisha kuwa addicted huyo du pole mdogo wangu.Mimi kama mwanaume ninachukia sana mambo ya sherehe za usiku hasa kwa wanafamilia zenye watoto kila weekend kukimbilia visherehe hivyo.Pia hali ya uchumi ilivyo unashangaa mtu unamaliza pesa zote kwenye michango.Pawepo na tahadhali na umakini wa kutumia pesa na si kila mtu anakuhusu.Siku hizi watu wameanza hata udanganyifu, utaona mtu kapewa kadi ya kuchangia arusi.Badala ya kuchanga yeye anaanza kusaka watu wa kumchangia halafu anakusanya pesa nyingi ambazo wala hazipeleki huko anatoa kiasi kidogo tu nyingi zinabaki kuwa myaji wake.Mimi nimekataa michango ya arusi na nimewaambia jamaa zangu kuwa niitwe kwenye ugonjwa, elimu, misiba au ujenzi, na siyo kuchangia harusi maana harusi ni kwenda kanisani basi ndoa inafungwa wahusika waendelee na maisha kama wanahitaji sherehe wanaweza kuweka sherehe ndogo isiyo na gharama.Huyo mkeo mkalishe mhesabie moja na mbili hadi tano alijue hilo kwamba hataweza kwa mtindo huo.
Hiyo tabia sio nzuri kwani wamama wengi wanakimbia majukumu na kujifanya wako busy na shunguli za watu.shughuli ambazo ni za matumizi yasio ya lazima. mkalishe ongea naye mwelimishe wazi kuwa hali ya maisha ni ngumu sana na ikibidi kama yeye ni mfanyakazi atoe pesa zake kwenye hiyo michango na sio lazima kuhudhuria.
MSUYA HAPO JUU KAONGE VITU MUHIMU SANA INAELEKEA HUYO MKEO KAKUTAWALA HAIWEZEKANI KULA KITCHEN PARTY AALIKWE NA AEENDE KWANINI HUMWAMBII HAKUNA RUKSA NA AKAACHA KWENDA AU UMEMUACHIA UHURU MPKA ANAJISAHAU LAKINI KAM UNGEKUWA NAE MKALI SIDHANI KM ANGEKUCHEZEA MAANA HUKO NI KAMA KAMPATA FALA WAKE WAKUMCHEZEA..MIE HUO UJINGA KWA MCHUMBA WANGU TU HANIELEWI NIKISHA ENDA WEEK ILIYOPITA NEXT TENA NIMUELEZE HUO UJINGA SITHUBUTU...
Chapisha Maoni