Kwa wale wadau wa simulizi nitaendelea kuwawekea simulizi , kuna simulizi nilikuwa sijaziendeleza kama ya MAMA MDOGO, DADA YANGU ambazo zipo katika kitabu changu cha MALIPO NI HAPAHAPA zitaendelea kwa wale ambao hamkusoma mwanzo ingia katika kipendele cha SIMULIZI ZA KUSISIMUA katika blog hii utapata kusoma sehemu zote za simulizi . katika kitabu cha MALIPO NI HAPAHAPA zipo simulizi tatu na zote utapata kuzisoma na nyingine nyingi zinakujia soon tuendelee kuwa pamoja.
MALIPO NI HAPAHAPA SEHEMU YA KWANZA
Katika Mji
wa Arusha Mtaa wa Kaloleni ni eneo ambalo wakazi mbalimbali
walipendelea sana kuishi kutokana na mazingira yake kuwa tulivu na
yenye mandhari nzuri. Katika mtaa huo aliishi mzee mmoja aiitwaye
Magesa. Mzee huyo alikuwa na mke na watoto watatu, watoto wawili
wakiume ambao waliitwa Joseph na Peter na mtoto mmoja wa kike aliyeitwa
Julieth.
Mzee
Magesa hakuwa na uwezo mkubwa sana kifedha. Maisha ya Mzee huyo na
famila yake yalitegemea sana kipato kidogo kilichotokana na biashara
ya kuuza mboga sokoni ambayo alikuwa anaifanya siku zote za maisha
yake hadi akapewa jina la ‘Muuza mboga’. Mke wake alikuwa ni mama wa
nyumbani akijishughulisha na kupika chapati na kuuza ili kuongeza
kipato kwa ajili ya mahitaji ya pale nyumbani.
Maisha
yalikuwa magumu sana lakini familia ilikuwa na furaha na upendo kwani
waliishi kwa kupendana na kuheshimiana. Mzee Magesa aliwapenda sana
watoto wake, kwani mara nyingi alikuwa akiwafundisha mambo mbalimbali
kuhusu maisha ikiwa ni pamoja na kuwasisitiza kusoma. Julieth alikuwa
Darasa la Tano na mdogo wake Joseph alikuwa Darasa la Pili, Peter yeye
alikuwa hajaanza shule.
Siku moja
yapata saa mbili usiku Mzee Magesa akiwa amekaa kwenye sebule
karibu na chumba chake cha kulala alimwita Julieth kwa ajili ya mazungumzo.
“Julieth!”
Mzee Magesa aliita kwa nguvu. “Abee
baba!” Aliitikia Julieth aliyekuwa anaosha vyombo huku akimwendea
baba yake.
“Unafanya
nini saa hizi?” Mzee Magesa aliuliza kwa sauti ya upole.
“Naosha
vyombo baba.” Alijibu Julieth kwa adabu.
“Umemaliza?”
Aliuliza tena Mzee Magesa.
“Hapana
baba, bado sufuria mbili.” Alijibu Julieth.
“Acha
utamalizia kesho kaa hapo nina maongezi na wewe.” Aliongea Mzee
Magesa
huku akinyoosha kidole kwenye kiti cha miguu mitatu.
“Nimekuita
ili kukwambia maneno machache kuhusu hali ya maisha yetu
hapa
nyumbani.” Mzee Magesa alianza kueleza sababu ya wito huku
Julieth
akimwangalia na kumsikiliza baba yake kwa makini.
“Kama
unavyoona hali yetu ya maisha tunayoishi ni ngumu sana. Na hii
inatokana
na kipato chetu kuwa kidogo. Namna pekee ya kujikwamua na
hali hii
ni wewe mtoto wetu mkubwa kusoma kwa bidii ili uje utusaidie
sisi
wazazi wako pamoja na wadogo zako. Na pia …” Mzee Magesa
alikatisha
ghafla huku akiwa kama amekumbuka kitu fulani muhimu.
“Mama yako
yuko wapi?” Aliuliza Mzee Magesa.
“Yupo
chumbani.” Alijibu haraka Julieth.
“Mama
Julieth!” Aliita Mzee Magesa.
“Abee!”
Aliitikia mama Julieth kutokea chumbani huku akitoka.
“Mama
Julieth nina maongezi kidogo na Julieth naomba na wewe
ushiriki.”
Alitamka Mzee Magesa.
“Maongezi
gani hayo?” Aliuliza mama Julieth.
“Wewe kaa
usikilize ndio maana nimekuita”. Mzee Magesa alijibu kisha
akaendelea
kuongea na Julieth huku mama yake akiwa amekaa pembeni
mwa Mzee
Magesa.
“Julieth
kama nilivyoanza kukwambia maisha yetu ni magumu sana
kutokana
na kipato kidogo tunachopata. Tumejaribu kufanya bidii lakini
hakuna
mabadiliko. Njia pekee ya kujikwamua kiuchumi katika siku zijazo
ni elimu.
Hivyo wewe kama mtoto wetu mkubwa unatakiwa usome kwa
bidii sana
ili uje utusaidie sisi na wadogo zako pia. Sisi wazazi wenu
tutakazana
kuhangaika kutafuta fedha ili wewe usome. Angalia Mzee
Mtokambali
alisomesha mtoto wake wa kwanza hadi Chuo Kikuu, leo hii
wadogo
zake mmoja yupo Kidato cha Sita na mwingine Chuo Kikuu.
Maisha ya
Mzee Mtokambali ni mazuri. Ninaimani hata sisi hili
linawezekana
ilimradi tu kama wewe una nia ya kusoma.”
“Ni kweli
angalia mke wake anavyobadilisha kanga na vitenge, ni kutokana
na kijana
wao mwenye kazi nzuri. Baba Julieth, hili linawezekana mbona
binti yetu
ana nia sana ya kusoma na uwezo anao.” Alidakia mama Julieth
bila hata
kusubiri Mzee Magesa amalize.
“Baba na
mama nimesikia sana mawazo yenu mazuri ninapenda sana
kusoma.
Nitasoma!” Alisisitiza Julieth. “Julieth
wewe ndiye binti yetu wa kwanza, kumbuka wadogo zako bado ni wadogo
sana nakuomba mwanangu siku zote za maisha yako mtu asikudanganye
ukawachukia wadogo zako. Uwapende ndugu zako na kuwaheshimu
watu wote wanaokuzunguka wakubwa kwa wodogo, kwani mwanangu
kuna leo na kesho leo mimi na mama yako hatutakuwepo mshikamano
na upendo ndiyo silaya yenu.
Hata ukisoma sana kama hutawapenda
na kuwaheshimu wadogo zako na watu wote itakuwa ni bure.”
Aliongeza Mzee Magesa. Julieth
aliinamisha kichwa chini kama vile anatafakari kitu halafu akawaangalia
baba na mama yake kwa uso wenye maswali. “Baba
mbona mnaongea hivi? Mimi nawapenda wadogo zangu na watu wote, hata
siku moja haitatokea nikawachukia wadogo zangu. Lakini mbona leo
mnaongea hivi?” Aliuliza Julieth kutaka kudadisi zaidi.
“Huu ni
mwendelezo tu wa maongezi ambayo mara kwa mara mimi na mama yako
tumekuwa tukifanya. Ila leo tumeongea kwa msisitizo zaidi kwani
maisha ni magumu kupita siku zilizopita. Lakini pia kumbuka sasa umekuwa
mkubwa hivyo lazima tukwambie msimamo wetu juu ya maisha yetu, yako
na ya wadogo zako, au siyo mama Julieth!” Alifafanua Mzee Magesa
huku akimgeukia mama Julieth. “Ni kweli
wewe ndo mkubwa lazima uyajue haya kuanzia sasa ili kukujengea
uwezo wa kuishi vizuri na watu.” Aliongeza mama Julieth. “Sawa
wazazi wangu nimewaelewa.” Alisema Julieth.
“Baba Julieth
naona tumalize maongezi kwani kesho asubuhi na mapema
unatakiwa
uwahi sokoni kufungua biashara. Na wewe Julieth kesho ni
shule,
hebu tukalale.” Alishauri mama Julieth.
“Haya
Julieth nenda kapumzike ila ukae nayo kichwani yote
tuliyozungumza
leo.” Alisisitiza Mzee Magesa huku akisimama kuelekea
chumbani.
“Sawa
baba.” Alijibu Julieth. JE NINI KITAENDELEA USIKOSE SEHEMU YA PILI........
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni