Kumekuwa na ongezeko kubwa kila kukicha la kina dada
wanaojiuza katika maeneo mbalimbali, Na wengi ukizungumza nao na
kuwauliza kwanini wameamua kufanya biashara hiyo husema ni kutokana na
hali ya maisha kuwa magumu. Hivyo wanaona njia hiyo ni rahisi katika
kujiingizia kipato.Nilibahatika kuzungumza na binti mmoja ambaye
alionekana kuwa na umri kati ya miaka 15 hadi 17.
Msichana huyu alikuwa
akijihusisha na biashara ya ngono mwenyewe anasema "Niliamua kujiingiza
katika biashara ya ngono kutokana na wazazi wangu kufariki na hivyo
kukosa msaada kutoka kwa ndugu.Na kwa wakati huo nilikuwa naishi mkoani
Tabora, nikaamua kuja Dar es salaam kutafuta kazi. Nilihangaika sana
kutafuta kazi bila ya mafanikio.
Baadaye nilikutana na dada mmoja
ambaye nilikuwa nikiishi naye na ndiye aliyeniingiza katika biashara hii
ya ngono. Nilimuuliza changamoto anazokutana nazo katika biashara hiyo
akasema "Kwa siku moja ninaweza nikalala na wanaume zaidi ya watano,
kuna wengine hawapendi kutumia kinga, hivyo unakuta anakuongezea pesa
kidogo, lakini wengine wanakulazimisha hadi kufanya mapenzi kinyume cha
maumbile na ukikataa anakupiga na hela hakulipi,hizo ni changamoto
ninazokutana nazo.
Lakini wanaume wengine wanakulipa tu vizuri" Alisema
Binti huyo ambaye alionekana kuchoka sana.Nilimuuliza iwapo kama atapata
msaada ili afanye biashara nyingine aachane na kujiuza akasema
"Biashara hii inaniingizia kipato kwa haraka kwa siku naweza kupata kama shilingi elfu hamsini au laki moja kama biashara ikiwa nzuri, lakini kama nikipata kazi itakayonisaidia kujikimu kimaisha naweza kuacha biashara ya ngono. Kwasasa mimi sina ndugu na hakuna anayenisaidia zaidi ya biashara hii ya ngono.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni