Jumatano, Juni 05, 2013

NI JAMBO LA KUMSHUKURU MUNGU KUPATA MALEZI YA WAZAZI WOTE WAWILI BABA NA MAMA. KWANI KUNA WALIOTAMANI KUPATA MALEZI HAYO LAKINI HAWAKUYAPATA.

kuna waliotamani kupata malezi ya Baba na Mama lakini hawakuyapata kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo , Baba au Mama ametangulia mbele ya haki mtoto akiwa katika umri mdogo,Baba kumtelekeza mtoto na mama au Mama Kumtelekeza mtoto kwa Baba. Kuna mambo mengi yanayoweza kusababisha kukosa malezi ya Baba na Mama.

Kuelekea siku ya kina Baba duniani ambayo hufanyika kila mwaka siku ya jumapili ya wiki ya tatu ya mwezi wa sita. Ni vyema akina Baba wakakumbuka majukumu ya kulea familia ikiwa ni pamoja na kuwa karibu na watoto katika mambo mbalimbali. Kwani wengi huwa wanawaachia kina Mama pekee katika malezi ya mtoto .

Familia iliyonafuraha na amani na upendo ni familia inayoishi pamoja milele. LAKINI NI VYEMA KUMSHIRIKISHA MUNGU KATIKA KILA JAMBO.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom