Pages

Ijumaa, Agosti 02, 2013

MDHARAU MWIBA, MGUU HUOTA TENDE

Hivi wewe kaka unahadhi gani ya kuwa na mwanamke kama mimi. Embu jiangalie vizuri kuanzia chini mpaka juu halafu unitizame na mimi yaani huendani na mimi hata kidogo. Sulea Alikuwa akiongea kwa sauti kali sana huku akibidua midomo yake na kucheka kwa dharau.Kijana Vale alinyamaza kimya huku akionekana kuona aibu sana.Kwasababu palikuwepo na mkusanyiko wa watu eneo lile.


Akaamua kuomba samahani "Nisamehe Sulea, sikujua kama mimi kukutamkia nakupenda ingeleta tatizo kiasi hiki.Ni kweli mimi na wewe hatuendani asante sana nakutakia maisha mema" Aliongea Valle na kuondoka huku Sulea akiendelea kumrushia maneno "Kwenda zako kapuku mkubwa wewe,huna jeuri ya kumtunza mwanamke kama mimi, hahahaha usione vyaelea ujue vimeundwa, nenda katafute kapuku mwenzio.


Watu waliokuwepo pale wengine walicheka na baadhi wakionekana kusikitika sana "Mmh huyu mwanamke ana dharau jamani, halafu ana kauli chafu sana".
Baada ya mwaka mmoja kupita Sulea alipata mchumba ambaye alikuwa ni mfanyabiashara mwenye mali na pesa nyingi.Haikupita muda alibeba ujauzito baada ya kupata mimba yule kaka alimuacha bila ya kumsaidia chochote.Aliishi maisha ya tabu sana na ukizingatia alikuwa ni mjamzito. Kwani mchumba huyu alimuahidi kuwa angefunga naye ndoa lakini baada ya kupata ujauzito alimtelekeza.


Sikumoja akiwa anatembea huku na kule alisikia sauti ikimuita "Sulea, Sulea," Aligeuka na kumtizama alikuwa ni Vale ambaye alikuwa akiendesha gari aina ya Range Rover. Sulea alikuwa amechoka sana alinyamaza kimya kam mtu aliyepigwa na butwaa na kusema kwa upole "Vale, habari za masiku" Valle alimtizama na hakuamini kama ni Sulea yupo katika hali ile, alimuone huruma na kumsaidia. "Unaelekea wapi, naweza kukusaidia lifti," Sulea alipanda katika gari la Valle bila ya kusita.Akiwa ndani ya gari walizungumza mambo mengi sana.

 Sulea alimuomba msamaha Valle "Naomba unisamehe kwa yote niliyokutende nahisi hii ni adhabu ambayo Mungu amenipa katika maisha yangu.Kwani sina msaada wowote" Valle alimtizama na kusema "Pole sana, nakumbuka nilikupenda sana lakini haikuwa bahati yangu nashukuru Mungu kwa sasa nimeoa nina mke wangu na nampenda sana.Nitakusaidia pesa kidogo zikusaidie katika maisha yako. Sulea alibaki akiwa ameinama huku machozi yakimbubujika mithili ya mtu aliyemwagiwa maji.


Dharau ni mbaya sana, usimdaharau mtu kwa machache uyajuayo kuhusu yeye.Binadamu tunategemeana na kumbuka SIACHE MBACHAO KWA MSALA UPITAO.
 

MTUNZI...ADELA DALLY KAVISHE

Maoni 2 :

Bila jina alisema ...

adela hii story imenitouch utafikiri ni yangu nishawahi kupitia situation kama hii dah! imenikumbusha mbali sana asante sana kwa fundisho hii kweli usimdhau mtu awaye yoote hapa duniani

Bila jina alisema ...


NI KWELI BINADAMU TUNATEGEMEANA, SI KATIKA MAHUSIANO HATA KATIKA SHUGHULI ZETU ZA KILA SIKU

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom