KITABU- MALIPO NI HAPAHAPA
MTUNZI-ADELA DALLY KAVISHE
ILIPOISHIA
“Sawa
mimi nashukuru kama mmejipanga hivyo. Mungu akubariki sana
mimi
sina kipingamizi tena alimradi mmependana na kufuata taratibu za
kufunga
ndoa ili mpate baraka za Mungu. Pia ninaomba mkishaanza
maisha
muwe mnakuja huku kutusalimia mara kwa mara.” Mama Julieth
alishauri
huku akimkazia macho Julieth na baadaye John. “Hilo
halina tatizo kabisa mama hapa ni nyumbani tutakuja bila shaka kwani
nyumbani ni nyumbani, hata hivyo kwa sasa akishawaona wazazi wangu
tu atarudi ili kukamilisha mambo ya ndoa kama ulivyoshauri.” Alijibu
John.
INAPOENDELEA
Mikakati ya kuondoka ikaanza, mama Julieth akahamishwa kutoka
Mikakati ya kuondoka ikaanza, mama Julieth akahamishwa kutoka
nyumba
waliyokuwa wanakaa na kuhamia katika nyumba kubwa ambayo
ilikuwa
na kila kitu ndani. Kisha alitafutwa msichana kwa ajili ya kazi za
ndani.
Halafu nje ya nyumba alimfungulia duka dogo ambalo mama
Julieth
alikuwa akiuza bidhaa ndogondogo kama sabuni, sukari, unga na
vinginevyo.
Mwisho John alimnunulia mama Julieth simu kwa ajili ya
mawasiliano
ili kukitokea tatizo lolote atoe taarifa mapema. Mama Julieth
alifurahi
sana.
Siku
ya kuondoka ilikaribia Julieth alionekana mwenye huzuni kwa ajili ya
kumwacha
mama yake. Mama Julieth yeye alikuwa katika hali ya kawaida
akisisitiza
kuwa Julieth akumbuke yote aliyomwambia.
Safari
ya kwenda Mwanza ilianza hatimaye walifika salama na kwenda
moja
kwa moja nyumbani kwa John, maeneo ya Igoma. Julieth alishangaa
sana
kuona nyumba aliyokuwa akiishi John ilivyokuwa kubwa, nzuri na ya
kifahari
iliyojaa vitu vya thamani.
“Mpenzi
nyumba yako ni nzuri sana, yaani nyumba yote hii unakaa
mwenyewe?”
Aliuliza Julieth.
“Hapa
ni kwako mama, nilikuwa nakaa mwenyewe na vijana wa kazi lakini
sasa
nina mke aitwaye Julieth naamini nyumba hii itakuwa nzuri zaidi hasa
ikiwa
na watoto na mke mzuri kama wewe.” John alijibu kwa kiburi na
majivuno.
Julieth
alitabasamu huku akizunguka huku na kule akishangaa uzuri wa
nyumba
ile ya kifahari. John alipeleka mizigo chumbani na kumwelekeza
kila
kitu kilichomo na matumizi yake.
John
na Julieth waliishi maisha ya raha na furaha. John alimtembeza Julieth
sehemu
mbalimbali ili kumwonyesha utofauti wa mazingira ya Mwanza
na
Arusha. Katika kuishi kwake Arusha Julieth alikuwa hajawahi kufika
Mwanza,
aliupenda sana mji wa Mwanza hususan samaki aina ya sato na
sangara
wanaopatikana katika mji huo ambao huvuliwa katika Ziwa la
Viktoria.
Kwa ujumla Julieth alifurahia sana maisha yake mapya.
Baada
ya wiki moja kupita Julieth alitaka kuwafahamu wazazi wa John,
lengo
kuu la safari yao ilikuwa kwanza kwenda kuwafahamu wakwe zake.
“Vipi
mpenzi lini tutakwenda nikawafahamu wakwe?” Aliuliza Julieth.
“Usijali
mpenzi wangu tutakwenda tu kwani una wasiwasi gani, si upo na
mimi
kuna kazi tu zimenibana kwa sasa ila tutapanga mapema wiki ijayo.”
Alimjibu
John.
“Sawa
John hakuna tatizo nilikuwa nataka kujua ili nimjulishe mama
Arusha.”
Alijibu Julieth.
Mazungumzo
yaliendelea baadaye walichoka na kwenda kupumzika.
*****Baada
ya mwezi mmoja****
Wazazi
wa John walikuwa wakiishi Bukoba na siyo Mwanza kama John
alivyosema
akiwa Arusha. Kila mara Julieth alipomwambia suala la kwenda
kuwafahamu
wazazi wa John aliambiwa kuwa watakwenda asiwe na
wasiwasi.
Baadaye kutokana na raha alizokuwa anazipata Julieth, alijisahau
kabisa
kama hajafunga ndoa na John. Mama yake Julieth alipokuwa
akimpigia
simu na kumuuliza vipi kuhusu ndoa alimjibu hakuna tatizo
mipango
inaendelea vizuri. Kumbe ilikuwa ni uongo wao walikuwa
wakijirusha
na kusahau mambo ya ndoa na taratibu nyingine za kimila.
********Baada
ya miezi mitano**************
Baada
ya mapenzi na raha kushamiri, Julieth alipata ujauzito ambao
hakugundua
kama ana mimba. Aligundua baada ya kwenda hospitali
kupima
afya yake kutokana na kutojisikia vizuri ikiwa ni pamoja na kusikia
kichefuchefu.
Suala la mimba lilimfurahisha sana Julieth.
“Huu
ndio wakati mwafaka wa kufunga ndoa, najua John atafurahi sana
nikimzalia
mtoto. Akija leo nitamwambia tufanye haraka tufunge ndoa.”
Aliwaza
Julieth.
Ilipofika
jioni aliandaa chakula cha usiku mapema huku akiwa anamsubiri
mpenzi
wake arudi ampe taarifa kuhusu mimba aliyonayo. John alirudi na
kumkuta
Julieth anafuraha sana.
“Kulikoni
leo mpenzi mbona unaonekana una furaha sana kuna nini?”
Aliuliza
John.
“Mpenzi
leo nimetoka hospitali kupima nina ujauzito wako na sasa
nadhani
utakuwa muda mwafaka tufanye haraka tufunge ndoa.” Aliongea
Julieth
huku akitabasamu na kujichekeshachekesha.
”Ni
vizuri Julieth lakini kwanza ukisha jifungua ndio tutafunga ndoa.”
Alijibu
John akionyesha kutofurahishwa na taarifa ya Julieth kuhusu
ujauzito.
“Jamani
John ni muda mrefu tumekuwa pamoja kwa nini isiwe mapema
kabla
sijajifungua?.” Alisisitiza Julieth huku akimsogelea na kuweka
mikono
yake mabegani kwa John.
“Sikiliza
Julieth nikwambie; ndoa ina mipango mingi sana kwa hiyo wewe
nisikilize
mimi.” Alisema John huku akiwa anainuka na kuelekea
chumbani.
John
alikuwa kama mtu ambaye hajafurahia habari alizopewa na Julieth,
basi
Julieth alinyamaza kimya lakini aliendelea kufikiri na kutafakari hali
aliyoonyesha
John baada ya kupewa taarifa ya ujauzito.
“Mbona
John amebadilika ghafla kuna nini? Ngoja nimwache
nitamwambia
kesho vizuri.” Aliwaza Julieth huku akimfuata John
chumbani.
Kesho
yake asubuhi kama kawaida waliamka mapema sana, Julieth
aliandaa
chai. Walipokuwa wanakunywa Julieth alimwambia John kuwa
angependa
kwenda Arusha kuwaona mama na wadogo zake kwani ilikuwa
ni
muda mrefu.
“John
naomba niende Arusha nikamsalimie mama na wadogo zangu.”
Aliomba
Julieth.
“Huko
Arusha tutakwenda wote siku nitakayopanga mimi, tena nikipata
muda.”
Alijibu John akiwa amenuna.
“Vipi
John mbona umebadilika tangu jana naona haupo sawa tukiwa
tunazungumza
unaonekana una hasira kuna tatizo gani?” Julieth alihoji.
“Tatizo
ni wewe unaongea sana sipati hata muda wa kupumua, tena na hii
chai
kunywa mwenyewe.” Akaondoka na kumwacha Julieth akiwa
ameduwaa.
“Huyu
mwanamume amekuwaje mbona hivi jamani simuelewi.” Aliwaza
Julieth.
Basi
Julieth akaondoa vyombo mezani na kuendelea na shughuli zake.
Kadiri
siku zilivyozidi kusonga mbele tabia ya John ilizidi kubadilika.
Alianza
kuchelewa kurudi nyumbani na akirudi anakuwa amelewa sana,
tabia
hizo zilimuumiza sana Julieth kwani raha alizokuwa anazipata zote
aliziona
chungu na kujikuta akiwa mtu wa mawazo na kulia siku zote,
wakati
mwingine alikuwa akimpiga sana na alikuwa hataki kumsikiliza kwa
chochote.
Ilifikia
kipindi alimfukuza chumbani kwake akawa analala chumba cha
wageni.
John hakujali kama Julieth ni mjamzito alimpiga bila ya huruma,
kutokana
na matatizo kuwa mengi Julieth aliamua kumpigia simu rafiki
yake
wa kike aliyejulikana kwa jina la mama Janeth ili kuomba ushauri
kutokana
na matatizo aliyonayo.
Akiwa
anampigia simu alikuwa chumbani bila kujua kwamba John alikuwa
amejificha
pembezoni mwa mlango wa kuingia chumbani akisikiliza kila
kitu
alichokuwa anamwambia rafiki yake. Akiwa anaendelea kuongea na
simu
John aliingia kwa hasira sana na kumnyan’ganya simu kisha kumpiga
makofi
huku akizungumza maneno makali.
“We
shetani ulikuwa unazungumza na nani?” Aliuliza John kwa hasira.
“John
leo unaniita shetani? Halafu unanipiga?” Aliuliza Julieth huku
machozi
yakimlengalenga.
“Ndio
nani ulikuwa unamwambia mimi nakunyanyasa? We masikini
nakuuliza
mwendawazimu mkubwa na nitakuua leo na simu naichukua,
hutakiwi
kuwa na simu umekalia umbea tu. Nisikusikie unamwambia mtu
yeyote
mimi nakutesa mwehu wewe hata ukiwaambia watanifanya nini?”
Wakati
John akiwa anasema maneno yote hayo Julieth alikuwa akilia kwa
uchungu
wa maumivu.
“Unanionea
John nimekukosea nini mimi.” Alilalamika Julieth huku
akishikashika
na kupapasa tumbo lake.
“Nyamaza
sitaki kusikia sauti yako nasikia kichefuhefu kabisa toka hapa.”
Alisema
John huku Julieth akiondoka akiwa analia. Ama kweli usilolijua
ni
sawa na usiku wa kiza. Julieth hakujua kwa nini John amebadilika vile
ghafla
na kwamba nini kifanyike ili kumrudisha katika hali yake ya kawaida
ilikuwa
ni kitu kisichowezekana ilibidi awe mvumilivu na kujipa
matumaini.
Baada
ya siku kadhaa kupita hakukuwa na mabadiliko yoyote ila matatizo
yalizidi
kila siku ilikuwa ni ugomvi. Miezi kadhaa ilipita bila Julieth kuwa
na
mawasiliano na wazazi wake kwani alikuwa hana simu, hivyo ilikuwa
vigumu
kujua hata wazazi wake walikuwa wanaendeleaje. Kwa kweli
maisha
yalikuwa magumu sana. Wakati huo mimba ilikuwa na umri wa
miezi
saba lakini John alikuwa hajali.
Siku
moja John alimwambia Julieth kwamba siku zake za kuondoka
zinahesabika.
Ilikuwa ni yapata kama saa mbili usiku wakati Julieth
akiandaa
chakula cha jioni. John alifika na kumwita Julieth.
“We
mwehu si ulikuwa unataka uende nyumbani kwenu sasa muda wako
umefika
unaweza ukaondoka muda wowote nakupa wiki mbili tu.”
Aliongea
John kwa maneno ya kutukana.
“Lakini
si ulisema tutakwenda wote? Hebu niangalie na hali hii kweli ndiyo
niende
nyumbani mwenyewe. Afadhali nisubiri hadi nijifungue ndiyo
niende
nyumbani. “Wewe una kichaa nini hivi hapa ni kwako? Tena
sikiliza
kwa makini nataka uondoke uende popote unapopajua hata ukifa
shauri
yako. Kwanza hata hiyo mimba si yangu. Kwa hadhi yangu siwezi
kuwa
na mke kama wewe. Kwa taarifa yako mimi nina mke na mtoto na
siku
si nyingi anarudi sitaki aje akutane na kinyago kama wewe humu
ndani.”
John alitukana na kuongea kwa kebehi na dharau.
Akiwa
amejiinamia Julieth alisikiliza yale maneno na kuhisi kama ni ndoto.
Kabla
hajazungumza lolote John aliondoka na kumwacha akiwa na
mawazo
sana na kushindwa kuelewa mwenziwe ana matatizo gani.
Baada
ya wiki moja kupita tokea John alalame na kutukana wakati Julieth
akiwa
amekaa sebuleni mara John aliingia na kupita pale sebuleni kama
hajamwona
kisha aliingia ndani na kurudi na mabegi ya nguo na kumtupia
huku
akimfukuza Julieth aondoke na kwenda kwao.
“Kuanzia
muda huu ninavyoongea sitaki kukuona katika nyumba yangu tena.
Kama kuna kitu nimesahau kukitoa ukakitoe sasa hivi sitaki kukuona
hapa
mke wangu karibu atarudi.” Aliongea John kama mtu aliyepagawa.
“Jamani
mimi nitakwenda wapi na hii mimba? John uliniambia
unanipenda
kweli leo unanifanyia hivi? Nakuomba kama nimekukosea
unisamehe
unajua hali halisi ya maisha yangu nitafanyaje mimi kama
unanifukuza?
Je, maisha yangu yatakuwaje? Aliuliza Julieth kwa uchungu
huku
machozi yakimtoka kama mtoto mdogo.
“Mbona
siku uliponitoa kwetu ulionyesha kunipenda sana, halafu
ukamwambia
na mama….” Kabla Julieth hajamaliza kuongea machozi
yalimtiririka
mashavuni kama vile kamwagiwa maji kichwani.
“Mimi
nikupende wewe! Mjinga sana, nimekwambia ondoka kabla
sijakuua.John
”Alimfukuza Julieth na kutupa mabegi yake nje. Ilikuwa jioni
yapata
saa kumi na moja, Julieth alilia sana huku akiwa hajui atakwenda
wapi.
Aliondoka na kwenda nyumba ya jirani kidogo ambapo alikuwa
anakaa
rafiki yake aliyeitwa mama Janeth na kumsimulia mkasa mzima.
“Pole
sana rafiki yangu wanaume wa siku hizi ndivyo walivyo, mimi
nitakusaidia
ulale leo, halafu kesho uende tu nyumbani kwenu Arusha.
Nitakupa
hela kidogo.” Mama Janeth alimwonea huruma na kumfariji.
“Asante
sana mama Janeth kwani hapa nilipo sijui ningefanyaje.”
Alishukuru
sana Julieth na kwenda kulala baada ya kuonyeshwa sehemu
ya
kupumzika.. JE NINI KITAENDELEA USIKOSE MUENDELEZO WA SIMULIZI HII.
Maoni 4 :
Nzur sana.
Kwanini umeamua kuirudia hii stori mamii wakati ulishaiweka hadi sura ya 11? unatupoteza jamani bora ungeendelea pale ilipoishia.
Yaani wanaume ni mashetani
MDAU KUNA AMBAO WALIKUWA HAWAJAISOMA ILA NITAIWEKA HADI MWISHO WAKE
Chapisha Maoni