Pages

Jumapili, Oktoba 13, 2013

CHANZO CHA KUPIGWA RISASI MTANGAZAJI WA ITV UFOO SARO AMBAPO MAMA YAKE NAYE AMEUWAWA KATIKA TUKIO HILO

 Ilikuwa ni alfajiri siku ya leo maeneo ya Kibamba ambapo mtangazaji wa ITV Ufoo Saro, amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi  na mchumba wake ambaye baada ya tukio naye alijipiga risasi na kujiua.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa kipolisi Kinondoni, amedai kuwa mwanaume aliyetenda tukio hilo ni mchumba wake na Ufoo Saro na alikuwa anafanya kazi  katika Umoja wa Mataifa UN huko Sudan ila bado haijafahamika kitengo alichokuwa anafanyia kazi.


Kwa mujibu wa Kamanda Wambura inasemekana kulikuwa na ugomvi kati ya wawili hao ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa Mama mzazi wa Ufoo Saro ili awasuluhishe. 

Wakati wa usuluhishi tatizo lilionekana lipo kwa mwanaume. Mwanaume huyo alimshtumu Mama mkwe  wake kwamba amekuwa na mazoea ya kumtetea mwanae na ndipo alipoamua kutoa  bastola na Kumpiga Mama yake na  Ufoo Saro risasi ya kichwa  iliyosababisha kifo cha Mama huyo papo hapo. Pia alimpiga Ufoo Saro risasi ya mguuni na tumboni huku akifikiri kuwa ameshawamaliza wote na hivyo kuamua kujiua kwa kujipiga risasi ya kidevuni na kufariki papo hapo.


Inasikitisha sana jamani. Hasira ni hasara siku zote ni vyema kujifunza kuzuia hasira ili istokee matatizo kama haya ambapo kwa kiasi kikubwa kumekuwa na matukio kama haya na mengi ikiwa ni ugomvi wa kimapenzi. POLE SANA UFOO SARO MUNGU AKUPE NGUVU UPONE HARAKA . AKUPE NA UJASIRI KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU

HABARI NA ITV

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom