Jumanne, Oktoba 29, 2013

JE ULISHAWAHI KUWATENDEA MEMA WANAOHITAJI MSAADA KUTOKA KWAKO?

Kutenda wema ni jambo pana wala haliishi katika kusaidiana tu, bali linajumuisha  mambo mengi. ambayo binadamu humtendea mwenzake kuonyesha hisani, huruma na kuthaminiana.Wanafalsafa na wanasaikolojia wamethibitisha kuwa kila binadamu anastahili kuwa na furaha katika maisha bila ya kujali wewe ni mtu wa namna gani na una hali gani.

 Jambo la msingi ni wewe kukubalika na watu wengine kutokana na upendo ulionao juu yao yaani unawathamini na unawajali. Unapomuona mtu anashida lazima tujiulize je shida hiyo ningekuwa nayo mimi ingekuwaje? kwa kufanya hivyo unaweza kutambua kwanini mtu yule anahitaji msaada. Maisha yana mitihani mingi sana binadamu tuishi kwa kusaidiana kimawazo na vinginevyo kama vipo ndani ya uwezo wako.


Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom