Walimu ni watu muhimu katika kukuza sekta ya elimu nchini, kimsingi walimu mchango wao ni mkubwa katika kumpa mwanafunzi maarifa.Hii ni kutokana na kwamba wanafunzi wanakwenda shuleni wakiwa hawajui hili wala lile,lakini mwisho wa siku wanatoka vichwa vyao vikiwa vimeshiba maarifa ya kila aina. Hiyo yote ni kazi ya mwalimu.
Pamoja na Walimu kuwa na mchango mkubwa lakini wapo baadhi ya walimu wanatumia taalamu yao vibaya kwa kuwashinikiza baadhi ya wanafunzi ili wafanye nao mapenzi.Wanafunzi wanapogoma kufanya hivyo wanatengenezewa mizengwe ya kila aina na wakati mwingine kufelishwa kwa makusudi ili waonekane hawafai au wanafanya vibaya katika mitihani yao. Hii ni tabia chafu walimu wenye tabia hii waache mara moja.
Lakini pia wapo wanafunzi ambao wanapenda kuwaingiza walimu katika vishawishi kwa lengo lakutaka kufanya vizuri katika mitihani yao, hususani wanafunzi wa elimu ya juu (vyuo). Ni muhimu wanafunzi kujitambua na kuepukana na vitendo vya ngono ambavyo kwa kiasi kikubwa vinaathiri elimu ya yako.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni