KITABU -MALIPO NI HAPAHAPA
SIMULIZI -DADA YANGU
SIMULIZI -DADA YANGU
ILIPOISHIA
Baadaye James alikuja pale chumbani kwa Upendo bila taarifa, baada ya
kugonga mlango na kuruhusiwa kuingia alimkuta Grace akiwa amejilaza
kitandani akisoma gazeti.
“Habari gani dada!” Alisalimia James.
“Nzuri kaka karibu kiti.” Alijibu Grace.
“Asante dada. Aaahmm! Nimemkuta Upendo?” Aliuliza James huku
akitabasamu. “Ndiyo! Ila yupo nje amekaa chini ya mti mkubwa nyuma ya jengo hili.”
Alijibu Grace huku akiamka na kukaa vizuri kitandani.
“Haya asante hebu nimfuate.” Aliaga James na kuondoka. ITAENDELEA
INAPOENDELEA
INAPOENDELEA
Upendo alikuwa amekaa kwenye kiti cha plastiki huku amegeukia uzio
unaozunguka hosteli akichezea tawi dogo la mti. Mara James alikuja
kimyakimya akitokea kwa nyuma na kumziba Upendo usoni bila ya yeye
kumwona akiwa amebeba chakula kwenye mfuko. Upendo alishtuka sana
katu asijue ni nani aliyemziba macho.
“Nani tena jamani? Mimi huwa sipendi michezo ya hivi.” Alilalamika
Upendo. “Usiogope Upendo ni mimi.” James alitoa mikono yake na kumbusu
Upendo. “Waoo! James mbona hukunipigia simu kunitaarifu kama unakuja?”
Aliuliza Upendo huku akisimama kupokea mfuko aliokuwa ameubeba
James. “Nimekuletea chakula cha mchana Upendo.” Alitamka James bila kujibu
swali aliloulizwa. “Mmh! Nilijua ni watu wameamua kunichokoza. Asante sana kwa
kuniletea chakula, umejuaje James kwani mpaka saa hizi sijala njaa inaniuma kweli. Ehee! umeniletea chakula gani?” Aliuliza Upendo. “Fungua uone.” Alijibu James.
“Ooh! Chipsi na kuku napenda sana chakula cha aina hii, vipi njoo
basi
tule wote.” Aliongea Upendo kwa shauku huku akimalizia kufungua
mfuko.
Upendo alichukua maji ya chupa aliyokuwa nayo na kumwomba James
anawe mikono ili wale wote.
“Hapana mimi nimeshakula we kula tu usijali nimekuletea wewe.”
Alijibu
James huku akipokea chupa ya maji ili kumnawisha Upendo.
Akiwa anaendelea kula Upendo alikuwa ana mawazo mengi sana juu ya
James.
“Upendo napenda sana uwe mke wangu, kwa nini unaamua kuutesa moyo
wangu hivi?” Aliuliza James huku akimwangalia Upendo kwa kumtamani.
“Kwanini unasema nakutesa James nataka tu kuwa na uhakika kwani
naogopa sana kudanganywa.” Alijibu Upendo huku akimwangalia James
kwa kurembua macho.
“Niamini Upendo, mimi kamwe siwezi kukudanganya nakupenda kutoka
moyoni mwangu.” Alijibu James huku akimkazia macho upendo.
“Kweli James? Hata mimi nakupenda sana James ila...” Alisita Upendo.
“Ila nini.” Aliuliza James huku akiweka mkono wake begani kwa Upendo.
“Ngoja nije.” Aliinuka Upendo kuekelea chumbani kwake akimwacha
James akishangaa kulikoni.
Baada ya dakika kama tano, Upendo alirudi akiwa ameshika bahasha
mkononi iliyoandikwa “JAMES” ambayo aliiandika usiku ule, ili
wakionana ampe. James alimwangalia Upendo kwa mshangao asijue
chochote.
“James! Nimefikiria sana kuhusu ombi lako, nikatamani kukujibu usiku
kwenye simu, lakini ulimi ulinikwama nikashindwa kuongea. Hivyo
majibu
ya ombi lako yako humu.” Alimaliza kuongea Upendo huku akimkabidhi
James ile bahasha.
James alipokea ile bahasha huku mkono ukitetemeka kidogo na
kumwangalia Upendo usoni ambaye aliukwepesha uso wake na kuangalia
pembeni kwa aibu. Kisha akaamua kuifungua bahasha na kusoma
yaliyokuwemo ndani kwa makini huku akiinuka kumwangalia Upendo,
ambaye sasa alikuwa amefunika uso wake kwa viganja vyake vya mkono.
Haya ndiyo maneno aliyoyakuta James:
Mapenzi
ni matamu kama asali wawili tukipendana.
Mapenzi
ni machungu wawili tukisalitiana.
Mapenzi
ni zawadi daima tukipendana.
Mapenzi
ni lulu dhati tukipendana.
Mapenzi
ni kufa na kuzikana.
Nakupenda
Uwe
Baba!
Watoto!
Wangu!
Baada ya kumaliza kusoma ile karatasi James alimwendea Upendo na
kumnyanyua kisha akamkumbatia huku naye Upendo akizungusha
mikono yake na kumkumbatia James kwa nguvu kiunoni.
“Nashukuru sana mpenzi nakuahidi wewe ndio mke wangu.” Aliongea
James huku akiendelea kumrushia mabusu motomoto, huku naye Upendo
akijibu kwa kumbusu James ikiwa ni ishara ya kufungua ukurasa mpya wa
uhusiano wa James na Upendo.
************* Baada ya miezi sita ********************
Baada ya mapenzi kukolea James aliamua kumtambulisha Upendo kwa
wazazi wake. Baba na mama wa James walimpenda sana na kuwashauri
wafunge ndoa pindi tu Upendo akimaliza Chuo. Upendo alikuwa ndo
anaingia mwaka wa mwisho ili ahitimu katika shahada ya Sheria. Kadiri
siku zilivyozidi kusonga mbele James na Upendo waliyafurahia sana
mapenzi yao.
Ili kuimarisha zaidi uhusiano wao James alimwomba
Upendo waende kwa wazazi wake ili kutambulisha rasmi. Basi walipanga
safari ya kwenda Morogoro ambako walipokelewa vizuri sana na wazazi
wa Upendo. Baadaye wazazi wa Upendo waliwaasa juu ya uhusiano wao
kuwa usiathiri masomo ya Upendo. Wazazi wake Upendo walishauri
kwamba Upendo amalize Chuo kwanza na atafute kazi ndipo wafikirie
suala la kufunga pingu za maisha.
Wakati James akiwa Morogoro mdogo wake Upendo alikuwa chuoni.
Baada ya kukaa siku kadhaa Morogoro James na Upendo walirudi Dar es
Salaam. Kutokana na ushauri wa wazazi wa pande zote mbili maisha ya
James na Upendo yalikuwa ni ya furaha siku zote yenye mategemeo
mazuri katika kuleta maendeleo ya maisha yao ya baadaye.
Akiwa chuoni Upendo alisoma kwa bidii sana na James aliendelea na
biashara zake. Siku moja Upendo alimpigia simu mdogo wake na
kumwambia juu ya uhusiano wake na James.
“Haloo! Mambo mdogo wangu! Mzima wewe! Habari za Chuo?” Ilikuwa
ni sauti ya Upendo katika simu.
“Nzuri ndugu yangu mambo magumu sana chuoni, bora wewe
mwenzangu unakaribia kumaliza.” Alisema Eliza.
“We! Hakuna cha uafadhali wowote na hiyo mitihani inavyokuja migumu
nimetingwa ile mbaya. Kumbuka wewe si ulisema ukienda chuo utajirusha
sana. vipi imekuaje.” Aliuliza Upendo.
“Yaani, we acha tu ‘my sister’ (dada yangu) sina hata huo muda wa kujirusha
nikicheza mbona nitafeli mmh nipe umbea maisha vipi.” Alihoji Eliza.
“We nawe kwa umbea, Eliza mwenzio nimepata mchumba nikimaliza
Chuo naolewa.” Alisema Upendo huku akicheka.
“Usiniambie! Hongera mwaya, haya huyo shemeji anafanya kazi gani?”
Aliuliza Eliza.
“Ni mfanyabiashara na pia huwa anakuja Arusha mara kwa mara, nadhani
mtaonana au ukija likizo utamwona. Nyumbani nilishampeleka
kumtambulisha kwa wazazi.” Alieleza na kufafanua Upendo.“
“He! Kumbe mmefika mbali hivyo hata kuniambia mwenzio.” Alilalamika
na kulaumu Eliza.
Eliza huku akiwa na shauku ya kutaka kumfahamu shemeji yake, Upendo
akajitetea;
“Wala sio hivyo ‘my young
sister’ (mdogo wangu) mambo yalikwenda
harakaharaka lakini, utamfahamu na wewe ndiye utakuwa mstari wa mbele
kwenye harusi yangu.” Aliongea Upendo kwa majivuno.
“Haya bwana mimi nakutakia mafanikio mema Mungu awajalie mfikie
malengo yenu.” Alisema Eliza basi wakaendelea kuzungumza na baadaye
walikata simu na kuendelea na mambo mengine.
Kutokana na kazi kuwa nyingi za kusafiri mara kwa mara James alipata
safari ya kwenda Arusha kikazi. Wakati huo ilikuwa ni kipindi cha
mitihani
kwa Upendo basi, waliagana. Siku hiyo walikuwa pamoja ikiwa ni siku
moja kabla ya James kuondoka .
“Mpenzi wangu, utanikosea sana ukichelewa kurudi si unajua
nimekuzoea.” Aliongea Upendo kwa sauti ya mahaba.
“Usijali mpenzi ni kazi zinanifanya nisafiri nitawahi kurudi ila na
wewe si
una mitihani kwa sasa inabidi usome kwa bidii ili ufaulu vizuri sawa
mama?” Aliongea James huku akimsogeza Upendo kifuani mwake na
kumkumbatia.
“Sawa lakini si unajua sipendi kukukosa siyo uende huko ukanisahau
kwa kujirusha na vimwana vya Arusha.” Upendo alisisitiza.
“Ina maana huniamini mamii nakupenda sana hakuna mwanamke wa
kunidanganya wala usijali.” Alijibu James huku akitabasamu.
Walizungumza sana siku ile wakiwa nyumbani kwa James na baadaye
walikwenda kupumzika.
Kesho yake mapema saa mbili asubuhi James aliondoka na huku
akisindikizwa na mpenzi wake hadi uwanja wa ndege tayari kwa kuanza
safari. Baadaye Upendo alirudi chuoni kuendelea na masomo. Alipofika
Arusha James alikwenda moja kwa moja hadi katika hoteli ya Ngurdoto
yenye mandhari nzuri sana. Alipata chumba na baada ya kuingia kwenye
chumba chake alimpigia simu mpenzi wake kumtaarifu kuwa amefika
salama.
“Mambo mpenzi wangu! Nimefika salama nipo Hoteli ya Ngurdoto
natamani tungekuwa pamoja,” Aliongea James kutoka Arusha.
“Hata mimi pia natamani tungekuwa pamoja mpenzi, ila majukumu ndiyo
yanatubana. Hapa nilipo najisomea yaani hii mitihani inayokuja
inaniumiza
kichwa sana.” Aliongea Upendo kwa unyenyekevu.
Nakuomba usinisaliti mpenzi, najua kuna wanaume wengi
wanakufuatafuata. Ziba masikio yako usisikie neno lolote kutoka kwa
mwanamume yeyote. Alitahadharisha James.
“Mmh we nawe kwa wivu, nakupenda sana siwezi kufanya hivyo hata
siku moja.” Alijibu Upendo. ITAENDELEA
Maoni 2 :
story nzur dada,lakin nin hatma ya 'bado mimi' na kosa langu ni lipi?
Mzuri sana hii .
Chapisha Maoni