KITABU- MALIPO NI HAPAHAPA
SIMULIZI- DADA YANGU
ILIPOISHIA
Nakuomba usinisaliti mpenzi, najua kuna wanaume wengi
wanakufuatafuata. Ziba masikio yako usisikie neno lolote kutoka kwa
mwanamume yeyote. Alitahadharisha James.
“Mmh we nawe kwa wivu, nakupenda sana siwezi kufanya hivyo hata
siku moja.” Alijibu Upendo. ITAENDELEAINAPOENDELA
Baada ya mazungumzo kila mmoja aliendelea na mambo yake.
Akiwa Arusha James alianza kufanya kazi zilizompeleka akiwa na
marafiki
zake ambao ni wenyeji wa huko walizunguka sehemu mbalimbali ikiwa ni
wiki mbili tangu James aondoke Dar es Salaam. Siku hiyo ilikuwa ni
siku
ya Ijumaa muda wa saa mbili usiku ambapo James na marafiki zake
walikwenda katika matembezi maeneo ya Sakina.
Walipofika huko walikunywa sana pombe huku wakiwa wanafurahi
pamoja wakati huo walikuwa Sakina Bar, waliendelea kunywa hadi
ilipofika
saa tano usiku.
“Aisee washikaji kwa nini tusiende disko Triple
A.” James aliyekuwa
ameshalewa aliwashauri wenzake.
“Swadakta! Hilo neno! Washikaji twendeni disko sijaenda siku nyingi
sana
nadhani itakuwa safi sana.” Mmoja wao aliongea huku akionyesha ishara
ya kuondoka.
Walikubaliana na kuanza safari ya kwenda ukumbi wa Disko wa Triple A
ambao haukuwa mbali sana na mahali walipokuwa. Kabla ya kupanda gari
waliokuwa nalo James alichukua simu yake na kumpigia Upendo.
“Haloo mamii vipi umelala mamaaa!” Aliongea James.
“Safi mpenzi wangu nilale kwa raha gani niliyonayo? Hapa nilipo nipo
bize sana na maandalizi ya mitihani. Vipi uko wapi mbona nasikia
kelele?”
Alijibu na kuuliza Upendo.
“Nipo na washikaji tunafurahi mpenzi wangu. Mimi nakutakia usiku
mwema.” Alijibu James ambaye hakusema kama alikuwa anaelekea disko.
“Vipi James yaani huyo mwanamke amekubana mpaka umwambie
unakwenda wapi? Kweli ninyi ndiyo wale hata ukitaka kula utampigia
simu
na kumwambia unachokula. Aaa! hebu twendeni alishauri Rama mmoja
wa rafiki zake wapendwa wa James.
“Acha hizo Rama huyu mama watoto wangu na kuhusu disko
sijamwambia kwani ingekuwa balaa muda huu”. Alijibu James huku
akitabasamu.
Walipofika disko walikaa na kuendelea kunywa sana. Huko disko
kulikuwa
na watu wengi wakiwemo wasichana warembo sana ambao James na
marafiki zake walianza kutafuta wasichana wa kucheza nao. James
alisimama na kumfuata dada mmoja aliyekuwa amekaa karibu naye na
kumuomba wacheze. Yule dada alikubali na kusimama na kuanza kucheza
naye. Kama kawaida, katika kucheza kuna mambo mengi, wakiwa
wanacheza James alimshika yule dada mkono na kumsogeza pembeni
sehemu iliyokuwa haina kelele na kufanya mazungumzo naye.
“Mrembo umependeza sana, halafu unajua kucheza sijui unaitwa nani.”
Aliuliza James huku akimwangalia kwa makini yule dada usoni.
”Asante kaka mimi naitwa Esta.” Alijibu yule msichana huku
akitabasamu
na kurembua macho.
“Una jina zuri sana Esta kama ulivyo mwenyewe.” Alisema James huku
akimtazama Esta ambaye alikuwa akitabasamu.
“Mbona wewe hujaniambia jina lako.” Aliuliza yule msichana.
“Usijali mrembo mimi naitwa Juliasi.” Alijibu James.
Basi wakafahamiana na kuendelea kucheza pamoja baadaye James
alimwomba Esta waondoke pamoja naye Esta alikubali na kuondoka huku
akiwaacha marafiki zake bila hata ya kuwaaga. Walichukua teksi nje na
kuelekea katika hotelini, wakiwa njiani walikuwa wamekumbatiana kila
mmoja akimwambia mwenzake maneno ya kimahaba hadi walipofika
hotelini na kuingia chumbani. Wakiwa ndani James alikuwa amechoka
sana
kutokana na pombe alizokunywa. Lakini Esta yeye alikuwa amelewa
kidogo hivyo alimsogelea James na kumvua shati taratibu pamoja na
suruali yake kisha kumwacha akiwa katika bukta. Baada ya kumaliza
kumvua kila kitu alimpandisha kitandani James akawa ametulia kimya
kama vile amemwagiwa maji.
Naye Esta alivua nguo zake na kuziweka pembeni na kisha akamsogelea
James.“Juliusi we ni mwanamume mzuri sana nafurahi kuwa pamoja na wewe
haijawahi kunitokea nikamwamini mwanaume kwa haraka kama ilivyo
kwako nimekupenda naomba usiniache.” Esta aliizungumza maneno huku
akiwa anamshika katika paji la uso naye James taratibu alinyanyuka na
kuanza kumbusu Esta bila hata ya kuzungumza lolote huku akimkumbatia
na baadaye walilala usingizi wa pono.
Ilipofika asubuhi Esta aliamka na kwenda kuoga wakati James alikuwa
bado amelala usingizi mzito. Baada ya Esta kutoka bafuni alikaa
katika
sofa lililokuwa pale chumbani huku akiwa anamsubiri James aamke.
“Mmh sijawahi kupenda kiasi hiki huyu mwanamume sijamfahamu vizuri
ni siku moja tu lakini nimempenda sana naamini atakuwa ni mwanamume
wa maisha yangu.” Aliwaza Esta huku akimwangalia James.
Wakati akiwa anaendelea kuwaza mara ghafla James aliamka kutoka
usingizini na kukaa pale kitandani huku akionekana kuchoka sana.
“Habari za asubuhi Juliasi mpenzi wangu umelala sana”. Esta
alimsalimia
James.
“Jana nilikuwa nimekunywa pombe nyingi sana vipi unaweza ukaondoka
tu muda huu usijali mimi nipo sawa tu.” Alijibu James.
“Sawa mpenzi mimi nitaondoka kwani hata hivyo nilikuwa na kazi ya
muhimu naifuatilia ila naamini usiku tutakuwa pamoja nataka
tuzungumze
zaidi.” Esta alisema huku akiwa ananyanyuka na kumsogelea James kisha
kumbusu na kuchukua mkoba wake kuondoka kwa furaha sana. James
alichukua waleti yake na kutoa kiasi cha shilingi laki moja na
kumkabidhi
Esta.
“Nimefanya nini mimi nimemsaliti mpenzi wangu Upendo itabidi niwe
makini sana hiki kitu asikifahamu vinginevyo itakuwa balaa.” Aliwaza
James baada tu ya Esta kuondoka.
Basi James alinyanyuka na kwenda kuoga na baadaye aliendelea na kazi
zake kama kawaida. Ilipofika jioni Esta alimpigia simu James na
kutaka
kuonana naye. James alimtaka Esta aende hotelini usiku ili waendelee
na
huo mchezo huku James akiwa anafanya kwa siri Upendo asijue.
Ilipita kama miezi miwili hivi James akiwa bado yupo Arusha akiwa
anaendelea na shughuli zake na bado akiwa na uhusiano wa kimapenzi
kwa siri na Esta.
******************
Huko Dar es Salaam Upendo alikuwa mpweke sana kwani alikuwa
amemaliza mitihani ila hakwenda Morogoro alibaki Dar es Salaam na
alikuwa akiishi katika nyumba ya James Kinondoni. Wakati wote
walikuwa
wakiwasiliana na mpenzi wake vizuri. James alitakiwa kukaa Arusha kwa
muda wa miezi minne ndio shughuli zake zitakuwa zimekamilika, kwa
hiyo alikuwa akimtaka Upendo avumilie na waendelee na mikakati ya
kufunga ndoa ili punde akirudi tu wafunge ndoa.
Upendo aliendelea na mikakati ya harusi huku akishirikiana na wazazi
wake pamoja ili kuandaa sherehe ya kumuaga Upendo. Akiwa katika
mikakati ya harusi alimpigia simu mdogo wake ili kumjulisha mambo
yanavyoendelea.
Simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa lakini baadaye ilipokelewa.
“He! We Eliza mbona umechelewa kupokea simu?” Aliuliza Upendo.
“Mh dada samahani nilikuwa bafuni, ehe niambie.” Alijibu Eliza.
“Ndugu yangu natamani ungekuja huku unisaidie katika mipango ya
harusi yangu vipi mnafunga lini chuo?” Aliuliza Upendo.
“Makubwa! Kweli mapenzi yamepamba moto ndio unaolewa na huyo
shemeji hata simjui jamani?” Alihamaki Eliza. ITAENDELEA
Maoni 2 :
Mmmh! Mchezo Wa Usaliti Ndo Umeanza Sasa Hata Kwenye Majina! Julius Na James Wapi Na Wapi!
Mmmmmh! Patam hapo.....
Chapisha Maoni