Huenda tumewaona wengi wao kama mashujaa, vijana wa kisasa au hata dada zetu wanaokwenda na wakati, kumbe ni wagonjwa wa akili.
Unasikiliza taarifa ya habari jioni. Unasikia kuwa, mwanamume amembaka mtoto wa miezi mitatu. Unaihoji nafsi yako… ni jambo gani lililosababisha akafanya ukatili huo? Je, ni tamaa kali ya ngono?Wengine hudhani ni kisasi au imani za kishirikina na kwamba wahusika wametumwa.
Huu ni upotoshaji, lakini ukweli ni kuwa hayo ni magonjwa ya akili ya ngono ambayo yanawakumba asilimia 35 au zaidi ya Watanzania wote.Watanzania hawa wanaugua magonjwa haya kwa wakati mmoja na kusababisha madhara mbalimbali kijamii, kiuchumi na migogoro katika familia na katika uhusiano.
Watu wenye magonjwa haya, si lazima watembee wakiokota makopo, kuvua nguo au kuwa na nywele ambazo hazijachanwa.Hawa ni watu wa kawaida ambao tunafanya nao kazi, wenye uwezo mkubwa katika taaluma au pengine ni wazazi au hata walezi.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akili na mtaalamu wa waathirika wa dawa za kulevya, Augustine Godman anasema, magonjwa ya akili kwa ujumla wake yanaweza kuzidi 1,886 lakini yapo yale ya ngono ambayo pengine yana changamoto lukuki kwa mwanadamu hasa Watanzania wasiofahamu kuwa ni magonjwa ya akili.
|
Maoni 1 :
du hayo ni magonjwa ya akili ya ngono!
Chapisha Maoni