Nyawana Fundikira (Malkia wa Kinyamwezi) amefariki leo mchana nyumbani kwake alipokuwa akiishi na mumewe Kaisi baada ya kuzidiwa na Malaria kali, na Baadaye mwili ulipelekwa Mwananyamala Hospitali. Nyawana alikuwa muimbaji wa taarabu lakini pia ni mtangazaji wa kipindi cha AMBAA NA MWAMBAO kila siku ya jumamosi na jumapili kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi saa tatu usiku. PASSION FM DAR ES SALAAM.Nimefanya kazi na Nyawana kwa takribani mwaka mmoja alikuwa na juhudi sana kazini, mcheshi wakati wote tumefanya pamoja kipindi cha THE BIG SHOW akiwa anazungumzia filamu zetu kwa namna mbalimbali.
Msiba upo kwa baba yake maeneo ya Magomeni kwa Bibi nyau karibu na msikitini, Mwili wa marehemu utasafirishwa kesho jioni kwaajili ya mazishi nyumbani kwao Tabora alipozaliwa na kukulia Marehemu.
Sisi tulimpenda, lakini Mungu amempenda zaidi. Rest in Peace Nyawana Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amen.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni