Yalaiti mtu angekuwa anaonekana mahali alipo, yaani kwa asilimia kubwa watu wanaotumia simu ya mkononi husema uongo, mtu anaweza kukuambia yupo Kariakoo kumbe yupo Kimara. Embu fikiria labda umemuona mwenza wako katika mgahawa fulani, halafu hapohapo na wewe ukaamua kumpigia simu na kumuuliza "Uko wapi mpenzi wangu" Naye akakujibu "Nipo nyumbani nimekaa naangali tamthilia" Huku ukiwa unamuona. Je ni kitu gani utakifikiria akilini mwako moja kwa moja itakupelekea kumuona mpenzi wako si muaminifu ndiyo maana amekudanganya. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni