Jumamosi, Novemba 16, 2013

USIFURAHIE KUANGUKA KWA MWENZAKO, WASAIDIE WENZAKO WAFANIKIWE

Ikiwa umebaki mwezi mmoja na siku chache kumalizika kwa mwaka 2013. Tunatakiwa kutafakari  na kujitathmini kwa yale tuliyoyafanya mwaka huu. Lakini pia tunatakiwa kukumbuka kuwasaidia wengine  katika kukamilisha ndoto zao ikiwa ni katika masomo, kazi na mambo mengine. Unaambiwa usikatishe ndoto ya mwenzako kwa tamaa kwani binadamu tunaishi kwa kutegemeana.

 Unapowasaidia wengine ndivyo ambavyo unaweza kufanikiwa zaidi hata kwa kile unachokifanya. Jambo la msingi ni kwamba usiwawekee vikwazo wenzako wakashindwa kufanya kazi zao au kuishi kwa amani. Wasaidie wenzako wafanikishe ndoto zao. Tuachane na dhana ya kuchukiana au kufurahia matatizo ya yule mwenye shida. Upendo, ushirikiano ni nguzo muhimu katika maisha na mafanikio.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom