Jumatatu, Februari 03, 2014

MWANAMKE AUAWA KINYAMA CHANZO ALAMA M.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda, alisema tukio hilo la kinyama lilitokea mwanzoni mwa juma huko katika Kijiji cha Kisa wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa.

Taarifa zilizotolewa na polisi wilayani humo zilisema, mwanamke huyo alikuwa mke wa mtu na aliwahi kumtoroka mume wake na kwenda kuishi na mpenzi wake aliyetambulika kwa jina la Josephat Chinga (32) na siku chache baadae nako kwa mpenzi wake huyo hakuonekana ghafla na baadae ndipo alikutwa ameuawa.

Kamanda Mwaruanda alisema, kichwa cha mwanamke huyo kilikutwa ndani ya sufuria na pemezoni kulikutwa karatasi lililokuwa na ujumbe ambao baada ya kusomwa iligundulika iliandikwa na mmoja wa wauaji.

Mtu aliyeandika barua hiyo alifafanua aliandika ujumbe huo baada ya aliyewatuma kumuuwa mwanamke huyo kushindwa kuwalipa ujira waliyoahidiana hivyo kuamua kumlipua na kuorodhesha majina ya wote waliofanikisha mauaji hayo.


Mtu huyo alifafanua kwua aliyewatuma alikuwa na lengo la kuchukua viganja vya marehemu huyo kwani alikuwa na faida navyo kwa kuwa ilisemekana vilikuwa na alama ya ‘M’ angevipata angetenezea dawa ya utajiri.

Mtu huyo alifafanua kuwa, waliahidiwa kulipwa shilingi laki nne kila mmoja aliyefanikisha mauaji hayo.

Kufuatia tukio hilo tayari watu wanne wameshakamatwa na wako mikononi mwa jeshi la polisi

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom