Jumatatu, Machi 17, 2014
EMBU SOMA KISA HIKI "NILISHUHUDIA MUME WANGU AKIMBAKA MTOTO WANGU WA MIAKA 9.
Newala. Kutokana na kumwamini mumewe, Rehema Saidi, mkazi wa kijiji cha Rahaleo, Kata ya Mkunya Wilaya ya Newala mkoani Mtwara, hakuwahi kutia shaka pale alipomwacha na watoto, wakati yeye alipolazimika kutoka kwenda sehemu yoyote kwa ajili ya shughuli za kifamilia.
Rehema na mumewe Juma Malolo waliishi na watoto wawili; mwenye umri wa mwaka ambaye walimzaa pamoja na mwenye umri wa miaka tisa ambaye (Rehema) alimzaa kwa mwanamume mwingine kabla ya kuolewa mara ya pili.
Mwanamama huyu anasema aliishi kwa raha mustarehe na familia yake na katika mazingira ya kawaida, hakuwahi kuwaza kutokea kwa kitendo alichokishuhudia Agosti, 14 mwaka jana, pale alipomkuta mumewe (Malolo) akimbaka binti yake (jina tunalihifadhi).
Rehema anasimulia kwamba siku ya tukio alikuwa akitoka sokoni alikokwenda kuchuuza mbogamboga kwa ajili ya kupata fedha za kujikimu yeye na familia yake.
¡°Niliporudi nyumbani nilifungua mlango bila hata ya kubisha hodi kwa sababu ni nyumbani kwangu na wala sikuwa na hofu ya jambo lolote¡-sikuamini pale nilipomkuta mume wangu akiwa anambaka mtoto wangu, kwanza nilipigwa na butwaa, nikapandwa na hasira, nilimvamia na kuanza kumpiga Niliumia sana kiasi siwezi hata kuhadithia aina ya maumivu niliyoyapata,¡± anasimulia kwa huzuni.
Anabainisha kuwa baada ya hapo, alitoka nyumbani hapo kuwaita majirani ili waweze kushuhudia kitendo hicho, lakini aliporejea hakumkuta mumewe kwani alikuwa ameondoka na kibaya zaidi alichukua fedha zilizotokana na biashara yake Sh40,000 ambazo zilikuwa ndiyo akiba pekee aliyokuwa amebaki nayo.
Nilikwenda kwa baba wa mtoto kumwambia ili anisadie fedha ya kwenda mjini kutoa taarifa polisi lakini alisema hana fedha. Hivyo nilishindwa kwenda na hata hospitali kumpima, kwa sababu sikuwa na fedha tena ...nilibaki nyumbani huku nikilalamika kwa kitendo alichofanyiwa mwanangu,¡± anasema Mariam.
Anaeleza kuwa alikaa siku tatu bila kumwogesha binti yake kwa lengo la kutunza ushahidi wa kitendo alichofanyiwa na wakati huo alikuwa akitafuta fedha ili aende polisi na baadaye kumpeleka hospitali, lakini hakufanikiwa.
Mariam anasema baada ya siku tatu kupita huku akiwa amepoteza matumaini ya kupata nauli, alimwogesha mtoto huyo, hivyo ni dhahiri kwamba alipoteza ushahidi wa kitendo alichofanyiwa.
Ilikuwaje?
Rehema anasema siku ya tukio, Agosti 14 mwaka jana aliondoka nyumbani kwake saa 11 alfajiri kwenda shambani kwa Mzee Makwedu umbali wa kilomita tatu kutoka kijijini kwake, kununua majani ya kunde ili ayapeleke Mjini Newala kuyauza.
Anasema alimwacha mumewe na watoto wawili. ¡°Nilimuaga mume wangu na kumwacha na watoto wote wawili, kwa kuwa nilimwacha na mtoto mchanga wa mwaka mmoja niliamua kufanya haraka ili asije akaanza kulia wakati sijarudi,¡± anasimulia na kuongeza:
¡°Kwa hiyo nilikuwa nakimbia wakati wa kwenda na hata wakati wa kurudi, lakini nilichokiambulia ni hicho nilichokiona.
Anasema katika miaka miwili ya ndoa aliyoishi na Malolo hakuwahi kuwa na shaka juu ya binti yake, kwani alihakikisha anamtimizia mumewe mahitaji yote ya ndoa.
¡°Kama mwanadamu niliwahi kuwaza kwamba mume wangu angeweza akawa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine, lakini sikuwahi kufikiri kuwa anaweza kumgeuza binti yake kuwa ¡®mke mwenza wangu¡¯,¡± anasema Mariam.
Kwa upande wake binti aliyebakwa mwenye umri wa miaka tisa (jina tunalihifadhi), anakiri kwamba baba yake huyo wa kufikia amekuwa akimfanyia vitendo hivyo mara kwa mara, huku akimtisha kumchinja iwapo angetoa taarifa kwa mama yake au mtu mwingine yeyote.
¡°Alikuwa akinifanyia mara kwa mara, mama anapoondoka kwenda katika shughuli zake za biashara ya mboga, alikuwa ananiita na kuniambia njoo ndani tufanye mambo na kunikataza nisiseme nikisema atanichija,¡± anasimulia binti huyo.
Hija Ahmad ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Rahaleo, anasema alishtushwa na tukio hilo ingawa juhudi za kumnasa mwanamume huyo hazijazaa matunda hadi sasa.
Ahmad anasema binti huyo kwa umri alionao, anahitaji msaada wa matibabu ya kisaikolojia. ¡°Mtoto huyu kwa sasa ameathirika kisaikolojia kutokana na kuzomewa na wenzake, mara nyingi utamkuta amejitenga ¡-.nadhani unahitajika msaada wa kumtibu kisaikolojia,¡± anasema.
Katibu wa asasi ya kutetea haki za wanawake wilayani Newala (NEWORA), Mwanahamisi Fakihi anathibitisha kupokea taarifa za tukio hilo na kwamba jitihada zinaendelea kumsaka muhusika ili afikishwe mahakamani.
Ubakaji Newala
Mganga Mkuu wa Hospital ya Wilaya ya Newala, Dk. Yudas Ndungile anasema matukio ya ubakaji yameongezeka katika wilaya yao na takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2012 walipokea kesi saba za ubakaji na mwaka jana kesi 11.
¡°Matukio ya ubakaji ni hatari kwa afya za wabakaji na wabakwaji, unajua kuna maradhi ya ngono ikiwa pamoja na Ukimwi, pia watoto wanaobakwa husababishiwa madhara makubwa ya kisaikolojia, wito wangu kwa jamii iamke kupambana na vitendo hivi vya ubakaji,¡± anasema Dk. Ndungile.
Karani wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Newala, Maweda Samuel anasema mwaka 2012 walipokea kesi saba za ubakaji na kati ya hizo, kesi namba 134 ilivunja rekodi kwani washtakiwa watatu walitiwa hatiani kwa kumbaka mwalimu na wote walihukumiwa kwenda jela.
Samuel anasema kuwa mwaka jana kulikuwa na kesi 11 za ubakaji mojawapo ikiwa ni ileinayomuhusu mshtakiwa anayetuhumiwa kwamba alimlawiti mbuzi hadi kufa. Mshtakiwa huyo yupo mahabusu hadi sasa kutokana na jamii kutaa kumwekea dhamana kutokana na kuchukizwa na kitendo hicho.
Ofisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Newala, George Martin anasema vitendo vya ubakaji kwa watoto vinashamiri katika wilaya hiyo na kuhusisha na imani ya kishirikina kuhu akieleleza kuwa tiba yake ni kutoa elimu kwa jamii juu ya athari za vitendo hivyo.
¡°Kwanza jamii ishirikiane na polisi katika kuwafichua wahalifu wa matukio haya ili sheria ifanye kazi yake na kutoa fundisho kwa wengine,¡± anasema Martin.
Mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Magala anasema vitendo vya ubakaji havikubaliki ndani ya jamii na kusisitiza kuwa watakaobainika kujihusisha na tabia hizo watachukuliwa hatua za kisheria.
¡°Wananchi wasisubiri mambo yaharibike ili tulaumiane, wahakikishe wanatoa taarifa hata kama ni za siri polisi au mahala husika ili wabakaji wadhibitiwe,¡± anasema Magala.
Vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia ukiwamo ubakaji, vinaendelea kushamiri nchini licha ya kuwepo kwa sheria ya makosa ya kujamiana ya 1998 (SOSPA) inayotoa adhabu ya kifungo cha maisha jela au miaka isiyopungua 30 kwa mtu anayepatikana na hatia kwa kosa hilo.
Tafiti zilizofanywa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) zinathibitisha kwamba vitendo vya ukatili hususan ubakaji ni vingi katika jamii, chanzo kikuu kikiwa ni kuporomoka kwa maadili na athari za utandawazi.
CHANZO MWANANCHI
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni