Kila mwaka ifikapo tarehe nane mwezi wa tatu, Duniani kote wanadhimisha siku ya wanawake, Mikoa yote nchini Tanzania imetakiwa kufanikisha siku ya wanawake. Madhumuni ya siku hiyo ni ni kutoa fursa ya kupima utekelezaji wa maazimio, matamko na mikataba ya kimataifa, kikanda na kitaifa inayohusu masuala ya maendeleo ya wanawake na usawa wa kijinsia. Kwa mujibu Katibu Mkuu wa Wizara ya maendeleo ya Jamii, jinsia na Watoto, Anna Maembe kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Chochea mabadiliko kuleta usawa wa kijinsia". Jamii itachochea mabadiliko ya kuachana na mila na desturi zenye madhara. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni