Alhamisi, Machi 13, 2014

MKASA MZIMA KUHUSU WEMA NA AUNT EZEKIEL KULA KICHAPO

Na Imelda Mtema na Gladness Mallya
KIMEWAKA! Habari zilizothibitishwa zinaeleza kuwa, sura mbili za mauzo kwenye sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel Grayson wanadaiwa kula kichapo kutoka kwa msanii mwenzao, Adam Kuambiana, Amani limeinyaka.

Tukio hilo lililoshuhudiwa na ‘shushushu’ wetu lilijiri mchana kweupe maeneo ya Mikocheni, Dar, hivi karibuni baada ya kuibuka timbwili lenye ujazo wa kilo kadhaa baina ya mastaa hao.

ALIANZA WEMA
Kwa mujibu wa chanzo, Wema ndiye aliyeanza kummwagia Kuambiana maneno ya shombo akimwambia kuwa ahakikishe siku hiyo haipiti bila kukata kucha za miguuni kwani ni ndefu na zinatisha.
“Mwanzoni ilikuwa kama utani tu. Wema alimwambia Kuambiana akate kucha, tena itabidi atumie mkasi wa kukatia michongoma maana kwa wembe hazikatiki.

“Pia Wema alimwambia yeye hawezi kumwacha mpenzi wake na kucha ndefu kama hizo za Kuambiana,” kilisema chanzo chetu.
Ilizidi kudaiwa kwamba wakati Wema akiendelea ‘kumpaka’ Kuambiana, Aunt aliyekuwa amejilaza chini alidakia na kusikika akisema kuwa ni kweli msanii huyo mwenye uwezo wa juu katika fani anatakiwa kukata kucha hizo huku akizungumza maneno ya shombo kwa jamaa huyo.

HASIRA
“Baada ya kuona imekuwa ‘too much’, Kuambiana alipandwa na hasira, akanyanyuka kwenye kochi na kumfuata Wema kwa lengo la kumpa kipigo,” kilisema chanzo hicho.


MARTIN KADINDA AMUOKOA
Habari zilidai kwamba, Kuambiana alipomfikia Wema alianza kumpiga vibao hadi meneja wake, Martin Kadinda akaingilia kati kumuokoa mwanadada huyo ambaye pia ni meneja wake.

KIBAO CHAMGEUKIA AUNT
Chanzo kilieleza kwamba baada ya kuachana na Wema, msaanii huyo ambaye pia ni ‘dairekta’ wa sinema mbalimbali za Bongo alimfuata Aunt na kuanza kumlamba makofi ya kutosha.
Tukio hilo lilizua tafrani na kuwafanya wasanii wengine waliokuwa eneo hilo wakimbie na kushindwa kuwatetea Aunt na Wema kwa kuogopa kugeuziwa kibao.
KUAMBIANA ANASEMAJE?
Baada ya kuinyaka ishu hiyo, mapaparazi wetu walimtafuta Kuambiana na kumuuliza kulikoni kugeuka bondia na kuwapiga warembo hao ambapo alikiri kutokea kwa ishu huyo.
Alisema kuwa, Wema na Aunt ni kama wadogo zake, tena yeye kama dairekta wao walipaswa kumheshimu na siyo kumvunjia heshima.

“Akina Wema ni wadogo zangu, wanahitaji kuniheshimu na mimi ndiye mwongozaji wa filamu yao, kwa nini wanikosee heshima? Hata kama wamekasirika lakini nimewashikisha adabu,” alisema Kuambiana kwa ile sauti yake nzito.

WEMA & AUNT
Kwa upande wao, walipoulizwa Aunt na Wema kuhusiana na kichapo walichopewa walisema walishamzoea jamaa huyo, lakini kwa alilolifanya la kuwapiga makofi  aliwakwaza kwa sababu hata kama ni mwongozaji wa filamu yao lakini alikuwa pale kwa ajili yao.

HISTORIA YA KUAMBIANA
Ukiachana na tuki hilo, Kuambiana anadaiwa kuwa na mkono mwepesi hasa anapokuwa ‘lokesheni’ ambapo mwaka jana, aliwahi kumtia mikononi staa mwingine wa filamu za Bongo, Rose Ndauka walipokuwa wakirekodi filamu visiwani Zanzibar.

Siku ya tukio hilo, Kuambiana alikuwa akidairekti Filamu ya Distress in Zanzibar. Alimshutumu Rose kuvaa mavazi tofauti na maagizo yake, katika kujibishana akamuwasha makofi.

HATA MITAANI!
Juni, mwaka jana, Kuambiana alimshushia kipigo Fadhili Joseph ambaye alimdai fedha za bia alizokunywa kwenye baa yake, Sinza, Dar es Salaam.
Kuambiana aliposhindwa kulipa aliacha laptop (kompyuta mpakato), siku iliyofuata alirudi na kushusha kichapo huku akiitaka laptop hiyo.

Kuambiana alikamatwa na Polisi Kawe, Dar kwa faili la malalamiko KW/RB/5761/2012 SHAMBULIO. Kesi hiyo ikahamishiwa Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ kwa vile ndiyo kituo cha karibu na eneo la tukio.

MADAIREKTA WAKOJE?
Mbali na Kuambiana, staa mwingine ambaye pia ni dairekta wa muvi za Bongo, Issa Musa ‘Cloud’ naye aliwahi kutoa kipigo cha bakora kwa msanii Blandina Chagula ‘Johari’ kwa kosa la kuchelewa kufika sehemu ya kurekodia filamu.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom