Pages

Alhamisi, Machi 20, 2014

UKATILI HUU KWA WATOTO HADI LINI "MTOTO ABAKWA KISHA KUVUNJWA SHINGO"


Mtoto wa miaka 13 amekufa wilayani Tarime baada ya kubakwa na kisha kuvunjwa shingo na mtu anayedaiwa kuwa ndugu yake. Mwanafunzi huyo wa shule ya msingi Nyangoto kata ya Matongo Nyamongo, alifanyiwa unyama huo juzi mchana katika kijiji cha Nyangoto. Mtuhumiwa Nyamatese Mkoma, licha ya  kudaiwa kumvunja shingo pia inadaiwa alimvunja paja la kulia kabla ya kumsababishia kifo. Polisi inamsaka mtuhumiwa. 

Kamanda wa Polisi wa Tarime Rorya, Justus Kamugisha amesema Mkoma alionekana mara ya mwisho akiwa ameongozana na mwanafunzi huyo na baadaye mwili wa mtoto ulikutwa vichakani. Kwa mujibu wa Kamanda, inadaiwa mtoto huyo alivunjwa viungo vyake kwa kile kinachosadikiwa kulikuweko na purukushani wakati akipambana kujiokoa. Mtuhumiwa alitoroka baada ya kufanya unyama huo. Tunamsaka mtuhumiwa huyo. Naomba wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi letu la Polisi ili tumkamate afikishwe katika mkono wa sheria. Alisema Kamanda. CHANZO HABARI LEO.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom