Katika jamii yetu wapo baadhi ya wazazi wasiojali umuhimu wa elimu na unakuta wanawaoza binti zao na ndiyo hao ambao hushirikiana na wanaume wanaowapa mimba mabinti zao. Ni vyema watu wa aina hii wakasakwa na kuchukuliwa hatua za kisheria , kwani serikali imekuwa ikijitahidi kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa elimu kwa watoto wote. sasa mtoto wa kike anapoharibiwa maisha yake kwa kupewa mimba ama kuwatafutia wanaume siyo vizuri.
Tena unakuta mzazi anajinadi "Yaani mwanangu nimemtafutia mwanaume ana pesa, ananisaidia kila kitu" Bila hata aibu wala huruma unakuta mzazi anafurahi mtoto wake kupata mwanaume. Na inapotokea mtoto amepata ujauzito wamo baadhi ya wazazi ama walezi ambao kutokana na umasikini wao huamua kunyamaza kimya baada ya kupewa chochote na wale wanaowapa ujauzito watoto.Ipo haja ya serikali kuangalia hali halisi ya maisha ya watanzania na hasa waishio vijijini kwani ndio wanaokumbana na vitendo hivyo, wakisaidiwa kuondokana na umasikini hawatakuwa tayari kupokea fedha haramu. NA MDAU, MKEREKETWA WA ELIMU.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni