Pages

Ijumaa, Aprili 25, 2014

Maoni ya mdau "Watanzania waachiwe wachague Serikali wanayoitaka


Mtanzania ambaye hajaelewa yanayoendelea bungeni hadi leo hii hatakaa aelewe tena. Bora rasilimali ya mahakama ingetumika kutafuta ufumbuzi wa hili. Sina Shaka, Mahaka itaamuru Bunge la Katiba lisitishwe kupisha kura ya maoni ifanyike ili watanzania waamue wenyewe serikali ya muungano wanayoipenda. Hakuna haja ya kupoteza muda wa rasilimali nyingi kuzunguka nchi nzima kuwaelewesha watanzania wanaoelewa tayari kuhusu yanayoendelea Bungeni. 

Chaguo lao lilikuwa serikali tatu wakipewa serikali mbili wataikataa  kwenye kura ya maoni Mambo mengine ni upotevu wa fedha muda na uharibifu wa fikra. Shime tuamke, Tujue Watanzania wanachokitaka . Hekima zitumike zaidi, katiba ni moyo wa Watanzania. Na Ama Masawe Dodoma

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom