Ikiwa leo Bunge maalumu la katiba linaahirishwa. Na hatua hii inafikiwa baada ya kumalizika kwa idadi ya siku zao za vikao vya awali zinazoainishwa kwenye Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Tunawatakia mapumziko mema wajumbe wote wa bunge maalumu la katiba , Hata hivyo tunawaomba kipindi chao cha mapumziko wasikae burebure, badala yake watumie muda huo kupata muda wa kutosha kujipanga upya kwa hoja zenye mashiko na wala si kujifunza namna mpya ya kumwaga kauli za kebehi na matusi dhidi ya wenzao kama ilivyodhihirishwa na baadhi yao katika mfululizo wa vikao vinavyomalizika leo.
Ni matumaini ya wananchi wajumbe hawa wakirudi watarudi kwa kasi mpya. Ni vyema pia wakatumia kipindi hiki kumaliza tofauti zilizojitokeza. Ni vyema wajumbe wakakumbuka kuwa ndoto ya Watanzania ni kuona Katiba mpya, tena inayikidhi matakwa ya waliowengi inapatikana. na wala siyo migogoro inayoweza kuwa chanzo cha kudumu kwa hali mifarakano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni