Alhamisi, Aprili 03, 2014

MIGOGORO YA MAPENZI YAZUA BALAA


Mwanaume mmoja nchini Kenya amewaacha wanakijiji cha Tivani Mkoa wa Rift Valley, vinywa wazi baada ya kujichimbia kaburi na hata kujaribu kujizika mwenyewe kutokana na alichosema ni matatizo ya ndoa. Mwanaume huyo alidai kuwa anamatatizo ya ndoa ambayo yeye mwenyewe ameshindwa kuyatatua na kwa hivyokwake kilichosalia ni kwenda mbinguni. 

Alisema mkewe amemwambia jambo ambalo lilimkera roho na ndio maana akaamua kujitoa uhai. Mwanaume huyo Kipsang alichimba kaburi hilo usiku na hata kujaribu kujizika akiwa hai wakati mkewe na watoto walipokuwa wamelala.

 Wanakijiji katika kijiji cha Tivan walikuwa na wasiwasi kuwa mwanamume huyo  alikuwa amerukwa na akili ingawa walikiri kuwa yeye na mkewe wamekuwa wakikumbwa na migogoro mara kwa mara. Mkewe alisema kuwa amechoshwa na mwanamume huyo ambaye ametelekeza familia na majukumu yake. Baada ya wanakijiji kumsihi huku wazee wakiwataka watu kupanda migomba ya ndizi eneo alilokuwa amechimba kaburi hilo ili kuzuia mikosi. CHANZO HABARI LEO.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom