Jumapili, Aprili 13, 2014

SWALI NA JIBU LA LEO "NIMEMPENDA TANGU TUKIWA SHULE , LAKINI HATAKI KUNIELEWA NIFANYEJE"

JIBU
Unapotafuta kitu chenye manufaa kwako, huwa hamna kuchoka wala kukata tamaa, na kama ukichoka tayari umekwisha kipata, Cha msingi ni kuendelea kumueleza shida yako na katika mazingira mazuri siyo mtu unakutana naye barabarani au unamtumia ujumbe na kumuambia nakupenda ni vyema ukaonana naye na kuelezea hisia zako, ili aweze kukuamini kuwa wewe si muongo.

 Tafuta siku na mahali pazuri ambapo unaweza kukutana naye na ukamweleza kwa kiasi gani unampenda, kwa hatua hiyo anaweza kukufikiria na kufahamu kwa kiasi gani unampenda. Lakini pia kuwa makini kuna mawili yawezekana akakubali au akakataa msikilize sababu zake ili wewe mwenyewe ujue kama tayari ana mtu mwingine au la. Ni vyema kuwa na moyo wa kukubali kushinda na kushindwa pale kunapokuwa na sababu za kufanya hivyo.

Unaweza kutuma maswali kupitia
 della.media@ymail.com

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom