Ijumaa, Aprili 11, 2014

TIBA YA MSONGO WA MAWAZO.


Msongo wa mawazo ni tatizo linalowakumba watu wengi, na tatizo hili husababisha watu wengi kupoteza maisha,Wanasayansi nchni China wameuamsha ulimwengu kwa mara nyingine baada ya kubaini kuwa chai ndiyo dawa kwa watu wanaotaka kuishi maisha marefu. Utafiti uliochapishwa kwenye jarida  la kimarekani la afya na maisha, ulieleza kuwa unywaji wa chai unasaidia kwa asilimia 10 kupunguza hatari ya kifo. 

Watafiti hao walionyesha kuwa kunywa chai mara kwa mara kunapunguza msongo wa mawazo, tatizo ambalo husababisha watu wengi kupoteza maisha.Hata hivyo utafiti huo ulionyesha  katika siku za karibuni sababu za vifo si hali mbaya ya kiuchumi pekee ama jisnia, umri au elimu bali ni baadhi ya tabia ikiwemo kula matunda na chai ya rangi. (green tea).

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom