Pages

Ijumaa, Mei 09, 2014

DINA MARIOS SASA AHAMIA KWENYE KIPINDI CHA TV,SOMA UJUMBE WAKE ALIOANDIKA INSTAGRAM


dinamariousNi miaka 8 sasa imetimia toka nilipokabidhiwa mtoto huyo.Nilimlea kwa taabu sana siku za mwanzo zilikiwa ngumu wakati mwingine sikulala kuhakikisha anakuwa salama.Nyakati hizo nilionekana nisingekuwa mama bora wa mtoto huyo lakini nilipigana kike na kuwa mtoto bora aliyependwa na kusifika nchi nzima.Mtoto huyo anaitwa leo tena na Dina Marios.Leo tena ikawa leo tena na kuwa kipindi bora kinachopendwa tanzania na dina marios nikawa mtangazaji bora wa kike na wapili bora Tz nzima kwa kupendwa hii ni kwa mujimu wa research.Kupitia leo tena nimetengeneza mashabiki,marafiki,wapenzi,na hata ndugu.Sasa leo tena imekuwa na sina budi kuiacha iendelee kulelewa na mtu mwingine.Kama nilivyokabidhia leo tena kuilea nimepewa tena jukumu lingine kubwa la kulea mtoto mpya atakaeonekana kwenye luninga inamaana ntakuwa nikiuza sura luningani.Niliwapenda sana wasikilizaji wangu japo mlikuwa mkiniuliza narejea lini kwenye leo tena ukweli ni kwamba sirudi tena kwenye leo tena.Naomba sala na dua zenu katika safari yangu mpya ambayo najua haitakuwa rahisi kama mlivyokuwa nami kwenye leo tena basi muwe nami katika hili.Wiki ijayo nitakuja rasmi kuwaaga kupitia leo tena ya clouds fm.Nawapenda mno *machozi kede kede yananimwagika*

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom